Home Michezo YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA, TFF YAMUAMURU DANTE KUREJEA KAZINI JANGWANI

YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA, TFF YAMUAMURU DANTE KUREJEA KAZINI JANGWANI

0

Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Tariq Seif Kiakala amewasili nchini kutoka Misri alipokuwa anacheza soka ya kulipwa kwa ajili ya kukamilisha mipango ya kujiunga na klabu ya Yanga.
Tariq Seif aliyekuwa anachezea klabu ya Dekernes FC ya Daraja la Pili nchini Misri ambayo alijiunga nayo msimu huu akitokea Biashara United ya Mara, amewasili leo nchini na kupokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, David Ruhago.

Katika hatua nyingine, klabu ya Yanga imeshinda rufaa dhidi ya beki wake, Andrew Vincent Chikupe ‘Dante’, ambaye ametakiwa kuripoti kazini mara moja.
Yanga walimkatia mchezaji huyo rufaa hiyo TFF baada ya Dante kugoma akishinikiza alipwe kwanza stahiki zake mbalimbali, ikiwemo fedha za usajili. 
Na baada ya tamko hilo la TFF, uongozi wa Yanga ukasema; “Uongozi wa mabingwa wa Kihistoria Tanzania,(Yanga SC) unamkaribisha tena kikosini beki @vicentandrew ‘Dante’ baada ya kumalizika kwa shauri la kesi baina ya pande mbili,”.