Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiifariji familia na waombolezaji mbalimbali kufuatia kifo cha Bi. Doleta Minya kilichotokea tarehe 09 Julai 2024. Makamu wa Rais ametoa pole hizo wakati alipoitembelea familia ya marehemu akiwa Kijiji Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma tarehe 11 Julai 2024