NA MWANDISHI WETU
TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), imemkabidhi mkandarasi kazi ya ujenzi mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Itipingi Mkoani Njombe ambao utagharimu zaidi ya shingi bilioni 5.2.
Mradi huo awali ulijengwa kwa gharama ya shilingi milioni 400.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ameiagiza halmashauri ya wilaya ya hiyo kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima wa na kutumia mradi huo ipsavyo.
Amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ya mradi mradi ikiwemo kupima mashamba na viwanja.
Pia, kuandaa teknolojia za kisasa za kilimo Pamoja na kuandaa masoko ya uhakika wa mazao yatakayo zalishwa kutoka eneo la mradi.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha itipingi Mtaka amewaasa wananchi kuutunza mradi huo kwa kuacha kupeleka mifugo katika eneo la mradi huku akionya vijana wanaojihusisha na kamari kuacha wizi wa vifaa na uvivu
Naye Mhandisi wa Tume Mkoa wa Njombe Machage Mwema, amesema baada ya usanifu wa pili,mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa baina ya serikali na mkandarasi kutoka kampuni ya Sihotech Engeneering Company ltd na Amj Global Multi contractor co ltd; June 24 mwaka 2024 jijini Dodoma.
Ameeleza shughuli ambazo mkandarasi huyo atafanya kwa kipindi cha miezi 14 ya ujenzi wa mradi kuwa ni Pamoja na kukarabati miundombinu iliyojengwa kwenye ujenzi wa awali,kundeleza na kujenga mfereji mkuu, kujenga mifereji ya umwagiliaji,kujenga bara bara za kuzunguka mashamba,ujenzi wa madaraja ,vivusha maji , kujenga bara bara kutoka eneo la mradi mpaka kijijini kwaajili ya kusafirisha pembejeo na mazao; na kujenga ofisi ya mhandisi wa umwagiliaji.
Pia amesema kutokana na ukubwa wa mradi serikali itanunua gari moja kwajili ya kuhudumia mradi na kwamba kazi ya ujenzi huo inaanza siku 14 baada ya mkandarasi kukabidhiwa kazi na kuwa mradi huo unalenga kuwahudumia wakulima 417, idadi ambayo inaongezeka kutoka wakulima 77 walio tarajiwa katika mradi wa awali.Wanufaika wa mradi watatoka vijiji vya Itipingi, Kiumba na Malombwe, halmashauri za makambako na Njombe.
Kwa upande wa wananchi wa Kijiji cha Itipingi wakiongozwa na diwani wa kata hiyo ya Igongolo Isaya Myamba, wameishukuru serikali kwa kutoa fedha za kujenga mradi huo kwa mara ya pili na wameeleza kiu yao ya kunufaika na mradi kwa kuzalisha mazao ya mboga mboga kwa wingi.