Msajili wa Vyama vya Siasa (RPP), Jaji Francis K. Mutungi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala ya Utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa leo tarehe 9 Julai 2024 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza akifafanua jambo mbele ya Viongozi wa Vyama vya Siasa wakati wa mafunzo ya viongozi hao kuhusu masuala ya Utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa leo tarehe 9 Julai 2024 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Washiriki wa mafyunzo haya ni Wenyeviti wa Taifa na Makatibu Wakuu, Maafis Manunuzi, Maafisa Hesabu, Watunza Kumbukumbu, na wataalamu wa mipango na bajeti wa vyama vya siasa.
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa wakifuatilia Mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala ya Utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa yaliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo tarehe 9 Julai 2024 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeandaa mafunzo ya siku mbili kwa upande wa Tanzania Bara kuanzia tareh 9 hadi 10, na baadae Zanzibar tarehe 15 na 16 Julai 2024 kwa lengo la kuwajengea uwezo vyama vya siasa katika kutekeleza utendaji wao baada ya kubaini mapungufu wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama lililoendeshwa na ofisi hiyo mapema hivi karibuni.