Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawati wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo wilayani Kilolo mkoa wa Iringa, Julai 8, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba na wa tatu kulia ni Mhandisi wa wilaya ya Kilolo Emmanuel Sagachuma ambaye alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha dirisha lisilokuwa na wavu katika jengo la utawala la Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo wilayani Kilolo Julai 8, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba na wa pili kushoto ni Mhandisi wa wilaya ya Kilolo, Emmanuel Sagachuma ambaye alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita kwenye bweni wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasicha Lugalo wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa, Julai 8, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo wilayani Kilolo mkoani Iringa, Julai 8, 2024. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja kati ya madawati yenye nyufa ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza kuwa aliyeyatengeneza ayachukue kwa gharama zake na atengeneze mengine yenye viwago na kuyarejesha katika Shule ya Secondairi ya Wasichana Lugalo wilayani Kilolo. Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa Shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa, Julai 8, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)