…………
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Angelah Kairuki (Mb)amelipongeza Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa kutumia mfumo wa dijitali ikiwemo matumizi ya teknolojia ya Uhalisia ulioongezwa (Augmented reality) na Uhalisia pepe ((virtual reality) kwenye kutoa taarifa kuhusu Urithi wa Asili na Utamaduni wa Tanzania.
Salamu hizo za pongezi zimetolewa leo tarehe 4 julai 2024 na Mkurugenzi Msaidizi wa Utalii Bw.Richard Wandwi alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kikao cha tathmini kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Mhe.Waziri, Mkurugenzi Msaidizi wa Utalii Bw.Wandwi, amebainisha kuwa matumizi ya teknolojia yanayowashirikisha wananchi ni ubunifu wa kupigiwa mfano huku akizitaka Taasisi nyingine za Wizara hiyo kuiga mfano ili kurahisisha utoaji wa taarifa kwa wananchi na watalii wanaotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.