Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (wa pili kushoto) akitembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa kitabu cha Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi (Citizen Budget) hatua inayoongeza uwazi kwa wadau.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (wa pili kushoto) akihoji kuhusu Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi (Citizen Budget), ambapo ameipongeza Wizara kwa uwazi na uwajibikaji, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akipewa maelezo kuhusu Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi (Citizen Budget) kutoka kwa Mchumi Mkuu wa Idara ya Usimamaizi wa Bajeti, Bw. Boniface Kilindimo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akipewa maelezo kuhusu Sera ya Fedha kutoka kwa Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. Fronto Furaha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akipewa maelezo kuhusu utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi hususani vijijini ili kuongeza uelewa kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Stanley Kibakaya, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akipewa maelezo kuhusu Usuluhishi wa Malalamiko ya kodi ili kuondoa changamoto kwa wananchi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST), Bw. Cherbin Chuwa, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akiagana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma, wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Shamim Mdee, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024, ambapo amewapongeza watoa huduma kwa umahiri wao katika kutoa elimu kwa umma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere (kushoto) akiondoka katika Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024, ambapo aliipongeza Wizara ya Fedha kwa uwazi na uwajibikaji kupitia Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi (Citizen Budget). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
………..
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa yaliyomo kwenye Bajeti ya Serikali kwa lugha nyepesi (Toleo la Mwananchi) kwa kuwa inamsaidia mwananchi kuielewa bajeti ya nchi.
Bw. Kichere ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kijitabu hicho ni sehemu ya uwazi na uwajibikaji kwa kuwa mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa mipango ya Serikali katika kutekeleza maendeleo yao.
Aidha, alisema kuwa watoa huduma katika banda hilo wanaonesha umahiri katika kuelezea masuala mbalimbali, jambo ambalo litasaidia kuongeza uelewa kwa umma kuhusu Sera na Majukumu ya Wizara.
Kwa upande wake Mchumi Mkuu wa Idara ya Usimamaizi wa Bajeti, Bw. Boniface Kilindimo, alisema kuwa Bajeti ya Serikali Toleo la Mwananchi ni kijitabu kinachotafsiri mipango na bajeti ya Serikali kwa muhtasari na lugha rahisi inayoweza kueleweka kwa mwananchi na wadau mbalimbali.
Alisema kuwa Kijitabu hicho kinasaidia kufahamu mipango na Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka husika na jinsi bajeti inavyoweza kutatua changamoto na kuhamasisha dhana ya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma.