Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mkazi wa Arusha aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nadhiru Nassor akimuhudumia mkazi wa Arusha aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Picha no.3 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama akimsikiliza mkazi wa Arusha mara baada ya kumfanyia kipimo cha kuangalia wingi wa sukari kwenye damu aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloyce Mohamed akimwelekeza matumizi sahihi ya dawa za moyo mkazi wa Arusha aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Afisa Muuguzi Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Mwenda akitoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Arusha waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Picha na JKCI