Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mh. Omary Kumbilamoto akipokea taulo za Diapers zilizotolewa na kampuni ya DRAFCO GROUP LIMITED kutoka kwa Afisa Rasilimali watu kutoka DRAFCO GROUP LIMITED Bw. Benjamin Mangi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Anatouglo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni 21,2024 kutoka kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mnazi mmoja Dkt. Linda Mutasa na Dr. Nelson Mabruki Kaimu Mganga Mkuu jiji la Dar es Salaam.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mh. Omary Kumbilamoto akikabidhi taulo za Diapers zilizotolewa na kampuni ya DRAFCO GROUP LIMITED kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mnazi mmoja Dkt. Linda Mutasa kushoto ni Afisa Rasilimali watu kutoka DRAFCO GROUP LIMITED Bw. Benjamin Mangi na kulia ni Dr. Nelson Mabruki Kaimu Mganga Mkuu jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mnazi mmoja Dkt. Linda Mutasa akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa shukurani zake kwa kampuni ya DRAFCO GROUP LIMITED.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mh. Omary Kumbilamoto akiishukuru kampuni ya DRAFCO GROUP LIMITED mara baada ya kupokea bidhaa hizo za taulo.
……………………..
Kampuni ya DRAFCO GROUP LTD imeushukuru uongozi
wa Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Ilala na Menejimenti ya Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa kutoa ushirikiano uliohitajika katika kufanikisha kampeni ya Mradi wa Diaper Care ambao umehitimishwa Juni 21,2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi katika kilele cha ukamilishaji wa Mradi huo wa Diaper Care katika hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Afisa Rasilimali watu kutoka DRAFCO GROUP LIMITED Bw. Benjamin Mangi kupitia mradi hu0 wa Diaper Care ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Juni 19 hadi Juni 21 2024)
Mangi amesema Kampuni ya DRAFCO GROUP imeweza kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Diapers, misaada ya bidhaa za Taulo kwa matumizi ya wagonjwa waliopo hospitalini wakiwemo watoto na watu wakubwa kama utekelezaji wa juhudi ya Kampuni za kuisaidia Jamii inayozunguka (CSR).
Sambamba na hilo, Mangi amongeza kuwa kampuni ya DRAFCO GROUP kupitia Mradi huu imetoa msaada wa Taulo zaidi ya 12,000 zenye thamani ya shilingi Milioni 10 {Kumi} kwa matumizi ya wahitaji zaidi ya 4,380. Kati ya Taulo hizo 12,000, Taulo 4,000 zilitolewa moja kwa moja kwa wahitaji 1,460 wakati wa Mradi, na Taulo 8,010 zitakabidhiwa leo kwa Uongozi wa Hospitali ambazo zinatarajiwa kusambazwa kwa wahitaji zaidi ya 2,920 kwa utaratibu utakaowekwa na viongozi.
Niwahamasishe, muendelee kutumia bidhaa za Taulo kwa matumizi ya
wamama, watoto na wagonjwa wenye uhitaji pia niwakumbushe kuwa bidhaa za Taulo ni nyenzo muhimu na ya lazima katika kulinda na kuboresha usalama wa mgojwa, mama na mtoto
Ninawahimiza kuwa kuweni mstari wa mbele katika kufanikisha suala hili na kuisaidia jamii kwa kuwapatia elimu mliyoipata kupitia Mradi huu ili mkuongeza uelewa kwa akina mama wengi zaidi juu ya matumizi ya taulo za Diapers.
Kampuni ya DRAFCO GROUP LTD ni watengenezaji wa taulo
za (Diapers) za BABY CHEEKY kwa ajili ya matumizi ya Watoto pamoja na CUIDADO na PINOTEX kwa ajili ya matumizi ya watu wakubwa, Wamama waliojifungua pamoja na Wagonjwa wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wake Meya wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mh. Omary Kumbilamoto ametoa rai kwa kampuni zinazozalisha bidhaa mbalimbali ambazo ni mahitaji muhimu kwa jamii kujitolea kutoa misaada kwa jamii ya wenye uhitaji.
Amesema msaada huo wa taulo za (Diaper) Cheeky Baby, Cuidado na Pinotex zilizotolewa na kampuni DRAFCO GROUP LIMITED ni muhimu sana kwa wahitaji na jambo jema ni kwamba elimu imetolewa pia kuhusu namna ya matumizi yake.
Amesema bidhaa hizo wamezipata bure na watahakikisha wanazitoa bure kwa wahitaji.
“Nikuhakikishie hivi vyote tutavitoa bure na nitoe rai kwa makampuni mengine kuiga mfano huu wa Kampuni ya DRAFCO wapo wengi wanaozalisha bidhaa kama hizi hapa nchini lakini hawana moyo wa kutoa”,Amesema Kumbilamoto.
Amesema Rais Dkt Samia amefungua milango kwa wawekezaji kuja kuweka viwanda nchini lengo likiwa wananchi wake waweze kupata ajira.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mnazi mmoja Dkt. Linda Mutasa ameishukuru kampuni hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana.
Amesema bidhaa hizo walizopokea wataziingiza kwenye mfumo wa kawaida wa hospitali na kuzitoa bila malipo kwa wahitaji.