Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hassan Kabeke,akitoa hotuba leo baada ya sala ya Eid Al Adhaa iliyoswaliwa kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza, Imamu Ayoub Abdallah (mbele), akiwaongoza Waislamu katika Ibada ya Sala ya Eid Al Adhaa, leo katika Uwanja wa Nyamagana.
Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka misikiti mbalimbali jijini Mwanza,leo wakiwa katika Ibada ya Sala ya Eid Al Adhaa iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana.
4.Pic namba 69-Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza,Imamu Ayoub Abdallah (mbele),akiwaongoza Waislamu katika Ibada ya Sala ya Eid Al Adhaa, leo katika Uwanja wa Nyamagana.
……
Pia,amewataka Waislamu na wasio Waislamu wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufinyika mapema mwaka huu.
“Nikiwa kiongozi wa dini nasikitika kuona Rais Dk. Samia akitukanwa na kudhalilishwa na baadhi ya vym vya siasa na wanasiasa wasio na maadili.Rais ni taasisi na Nembo ya nchi,hatizamwi kwa jinsia yake,dini yake ama kabila lake,ni Amiri Jeshi Mkuu anayesimama kama nembo ya nchi,”amesema.
Alhaji Kebeke amesema Rais Samia hatazamwi kama chama bali ni taasisi na nembo ya nchi,ni lazima na aheshimiwe na heshima yake ilindwe na Watanzania wote.
Kwa mujibu wa sheikh huyo wa mkoa tabia hiyo ikiendelea BAKWATA haitawaunga mkono viongozi wasio na maadili na vyama vyao,itawashauri waumini wake na wengine kuvikataa vyama hivyo na viongozi wao.
“Hatuzungumzii chama bali nembo ya nchi,hatuwezi kuunga mkono viongozi wasio na maadili ama sivyo tutawashauri waislamu wawakatae,”amesema kwa hisia kali na kuongeza kuwa;
“Mtu huyo unayemtukana na kumdhalilisha (Rais Dk.Samia),wakati unaumwa alikuja kukuona na hati yako ya kusafiria ina nembo ya Ikulu huku Kanda ya Ziwa tunamheshimu miradi mitano ya kimkakati ametekeleza kwa weledi,leo unamtukana hatuwezi kukubaliana na hilo.”
Sheikh Kabeke amewashauri viongozi wengine wa dini kukemea tabia hiyo ya matusi na udhalilishaji,ikiwezekana wawashawishi waumini wao wakikatae chama hicho na viongozi wake.
Akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu,amesema wenye sifa waislamu na wasio waislamu wakajisajili katika daftari la wapiga kura wakachukue fomu wagombee uongozi.
“Mwaka huu ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa wenye sifa na nafasi waende kwenye vyama wakajisajili,siku ya kupiga kura chagua kiongozi anayekufaa,usichague chama ama vyama visivyo na maadili,”ameshauri.
Kwa upande wa mmomonyoko wa madili Sheikh huyo wa Mkoa wa Mwanza,amesema dunia inalalamika kukosa maadili kwa sababu wanaopaswa kuyajenga yawezekana walikutana katika mitadao ya kijamii,facebook,whatsApp na twitter sasa X na unapotaka kuoa oa mwanamke mwenye dini anayemcha Mungu.
“Wapo watu leo hawawaheshimu wazazi wao,tunapomtafuta mtoto tumwombe Mungu atupatie mwenye maadili,maadili hayawezi kutengenezwa ndani ya umri wa miaka 30 na kiwanda cha kutengeneza watoto wema wenye maadili ni ndoa iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu,isiyotokana na kukutana kwenye mitandao ya kijamii,”amesema Sheikh Kabeke.
Aidha amewataka waislamu wasikubali kugawanywa kwa itikadi za dini zao,wajenge umoja na mshikamano ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii,bila umoja na mshikamano ni vigumu kuyafikia.
Pia amesistiza kulinda amani ya nchi akisema; “Ujumbe huu ufike, tuendelee kulinda amani ya nchi na bila amani leo tusingeswali hapa, dini yetu ni ya amani na mwislamu unapotembea unatangaza amani,tusikubali kuivunja amani yetu tuendelee kuilinda.”