Baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji mbalimbali Kata ya Rangwi Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga wakiwa katika mkutano na viongozi wao kujadili juu ya changamoto mbalimbali zinazoiwakabili ikiwemo adha ya maji ya muda mrefu
……………….
NA MUSSA KHALID
Wananchi wa Kata ya Rangwi Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wameilalamikia serikali ya Wilaya hiyo kwa kutowasaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama ambayo inawakumba kwa muda mrefu.
Wakifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi wananchi hao katika vijiji vya Dule,Nyigoi na Kweibuva na vijiji vingine vikiwemo Dukani,Mtimule,Kimgamoi,Nkeleo na Kijewa vikipata maji mara Moja kwa wiki.
Wananchi hao wamesema kuwa kutokana na ukosefu wa maji imepelekea waende umbali mrefu mpaka kilomita tano kutafuta maji huku wakitumia usafiri wa Pikipiki kwa malipo ya Shilingi 6000.
‘Tunakochotea maji kwenda ni mpaka Kilomita tano ambapo ni mbali sana kwani sisi ni sawa na hatupo Duniani na Hata maji tunayooshea vyombo hayafai kwa matumizi ya binadamu hivyo tunaiomba serikali yetu isikie kilio cha sisi wananchi wake’wamesema wananchi hao
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyigoi Abedi Iddy na Mkazi wa kijiji cha Veronika Moses Shemghande na Joyce John Kingazi,wamesema changamoto ya maji katika maeneo hayo ni ya muda mrefu jambo ambalo wamekuwa wakikumbana na magonjwa ya matumbo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Rangwi Seleman Lyimo amekiri uwepo wa changamoto hiyo kuhu akieleza kjuwa mradi huo ameshausemea kwa muda mrefu kwenye vikao bila ya kupata ufumbuvi licha ya kutengewa bajeti.
Amesema mradi wa maji alishausemea sana katika vikao vya madiwani na ulishatengewa bajeti kwa mwaka wa fedha uliopita Sh Mill 97 lakini haujatekelezeka kwa madai kuwa ni ndogo huku mwaka 2023/24 ukatengewa bajeti ya Mill 370,100,000 lakini hakuna utekelezaji uliofanyika.
Nimelazimika kumtafuta Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga Upendo Omary ambapo yeye amesema mradi huo mpaka sasa upo kwenye mkakati na utekelezaji wa wake unaendelea.
‘Nimewaahidi wananchi wa RANGWI kwamba nitafika ndani ya mwezi huu kabla ya kufunga mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kuangalia changamoto ya kipindi kijacho kwani utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utakwenda kufanyiwa ukarabati utafanyika pia katika kata hiyo’amesmea Meneya RUWASA
Amesema mikakati ya serikali ipo kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanafikiwa na maji hivyo wawe watulivu ikiwemo kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Japhari Mghamba amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha Kata ya Rangwi ipo kwenye mpango mkatati wa kujengewa miradi ya maji ikiwemo kuchimbwa kwa visima.
Amesema Kata ya Rangwi ni miongoni mwa kata ambazo zimeingia kwenye mradi katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai hivyo watakwenda kunufaika na mradi huo.
‘Ipo mikakati ya kwenda kuchimba visima karibu kumi ambapo hiyo kata ipo pia kwani ilishindikana gari kupanda kutokana na mvua na tunafahamu kuwa adha ipo lakini ipo mikakati ya serikali’amesema DC Japhari
Amewata wakati wa maeneo hayo kutambua kuwa serikali ipo na itahakikisha inatatua changamoto zao kupitia miradi miradi ya visima na miradi mikubwa ambayo imeingizwa kwenye mpango wa bajeti 2024/25