Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewahukumu Afisa Mtendaji wa Kata ya Iwindi na wenzake 2 kulipa faini ya Shilingi 500,000/= kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kupokea rushwa kiasi cha sh. 130,000/= kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na (2) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007.
Hukumu hiyo dhidi ya Bw Rubaha Mkwekwele Sonje, Bw Alex lauden Chawe na Bi Lenisa Raphael Simon katika shauri la jinai Na. 09/2023, ilitolewa Juni 10, 2024 na Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya. Mhe. Scout Peter Andrew.
Washtakiwa walifikishwa kizimbani kwa shtaka la kupokea rushwa kiasi cha sh. 130,000/= toka kwa mwananchi ili waweze kumpatia barua ya utambulisho wa kumdhamini ndugu yake aliyekuwa anashikiliwa kituo cha polisi Mbalizi.
Washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru.