MARUFUKU wafugaji kuingiza mifugo kwenye skim za umwagaji na mashamba ya wakulima ukikutwa kila mfugo utalipa kiasi cha shilingi laki moja(100,000) lengo likiwa epuka migogoro ya wakulima na wafugaji.
Akizungumza na wafugaji afisa tarafa ya Pawaga Emannuel Ngabuji alisema kuwa kumezuka wimbi la wafugaji kuwapiga wakulima kwa makusudi na kulisha mifugo yao mazao ya wakulima jambo ambalo halikubariki.
Ngabuji alisema kuwa wameweka faini ya laki moja kwa kila mfugo ili wafugaji waogope na wakatafute malisho sehemu waliyopangiwa na serikali na sio maeneo ya wakulima.
Alisema kuwa serikali imewekeza mradi wa skimu ya Pawaga wenye gharama ya bilioni 56 ambao unamanufaa makubwa kwa wakulima hivyo mfugaji ukipeleka mifugo kwenye skim utalipa faini na mifugo itataifishwa.
Ngabuji alimalizia kwa kusema kuwa serikali imewangia maeneo maalum ya wafugaji kufugia mifugo yao ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji hivyo mfugaji atakaye kaidi agizo hilo sheria itafuata mkondo wake.