Na WAF – Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu akielezea dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Afya ya kuanzisha Diploma ya juu kwenye masuala ya saikolojia tiba katika chuo cha Afya Mirembe ili kusaidia watu wenye changamoto za afya ya akili kutokana na ongezeko la idadi ya watu wenye changamoto hizo.
Waziri Ummy amesema hayo leo Juni 12, 2024 alipofanya ziara katika chuo cha Afya – Mirembe kwa kujionea hali ya chuo hicho pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa chuoni hapo.
“Tunaona ongezeko la idadi ya watu wenye changamoto za afya ya akili ambapo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa katika kila watu Nane mtu Mmoja ana changamoto za afya ya akili.” Amesema Waziri Ummy
Amesema, Afya ya akili sio uchizi ni kama changamoto nyingine ambapo kwa Tanzania kuna watu Milioni Saba wenye changamoto za Afya ya akili kati yao watu Milioni 1.5 changamoto zao zinatokana na Sonona ambayo inaongoza ikifuatiwa na matumizi ya dawa za kulenya.