Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akinyanyua juu hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. 

Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akionesha hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akimkabidhi hati ya ushindi Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumtangaza kuwa ndiye mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akisoma matokeo ya Jimbo la Kwahani. 

Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.

Aliyekuwa Mgombea wa CCM, Bw.Khamis Yussuf Mussa ‘Pele’ akifuatilia kwa makini utangazaji wa matokeo. 

Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.

Wananchi wakisubiri matokeo.
Waangalizi wa Uchaguzi wa Kwahani wakisikiliza matokeo.
*************

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani-Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad imemtangaza
Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa Kiti
cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
 
Mussa almaarufu Pele ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya kupata Kura 7,092 Kati
ya Kura halali 7,383 zilizopigwa na kuwabwaga wagombea wenzake 13 waliokuwa
wakichuana katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika tarehe 8 Juni,
2024.

Jimbo la Kwahani lilikuwa na wapiga kura

11,936 na waliojitokeza kupiga kura ni 7,522 ambapo kura 139 zilikataliwa hivyo
kufanya kura halali zilizopigwa kuwa ni 7,383.
 
Vyama 14 vilisimamisha wagombea katika
Uchaguzi huo mdogo wa kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini
Mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Wagombea wengine na kura walizopata katika
mabano ni pamoja na Bi. Jarade Ased Khamis  wa AAFP (06), Bi. Madina Mwalim Hamad wa ADA
TADEA (49), Bi. Shara Amran Khamis  wa ADC
(83), Bi. Zainab Maulid Abdallah  wa CCK
(21), Bw. Abdi Khamis Ramadhan wa CUF(79), Bw.
Bashir Yatabu Said  wa Demokrasia

Makaini (14) na Bi. Nuru Abdulla Shamte  wa
DP(07) .

Wengine ni Bw. Kombo Ali Juma  wa NRA (05), Bi. Mwanakombo Hamad Hassan  wa NLD (08),  Bw. Amour Haji Ali  wa SAU(07), Bi. Naima Salum Hamad  wa UDP(01), Bi. Mashavu Alawi Haji  wa UMD(05) na Bi. Tatu Omary Mungi  wa UPDP(06).


Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani umefanyika
kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),
Ahmed Yahya Abdulwakil (65) kufariki dunia mwezi Aprili mwaka huu.