Dkt. Joyce Nyoni (wapili kutoka kulia nyuma) akiwa katika picha ya pamoja ya washindi wa kwanza wa tuzo za uandaaji taarifa za hesabu kwa mwaka 2018
Dkt. Joyce Nyoni na Timu yake wakipita Kusalimia meza Kuu baada ya kukabidhiwa tuzo
Kutoka Kushoto Dkt. Joyce Nyoni Mkuu wa Taasisi, Dkt. Zena Mabeyo Kaimu mkuu wa Taasisi fedhaUtawala, CPA Aisha Kapande Mhasibu,CPA Manase Shunashu Mhasibu, Na nyuma CPA Athman senzota Mhasibu Mkuu
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akipokea Tuzo ya Mshindi wa Kwazna ya uandaaji taarifa za fedha kwa mwaka 2018 katika kundi la Vyuo vya elimu ya Juu,
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na timu yake wakifurahia ushindi wa Tuzo ya kwazna ya Uandaaji wa taarifa za hesabu 2018.
*************************************
Na Mwandishi Wetu;
Taasisi ya Ustawi wa Jamii imenyakua nafasi ya kwanza na kupata tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla iliyofanyika Disemba 7, jioni katika viwanja vya NBAA Bunju.
Kwa mara ya nne mfululizo Taasisi ya Ustawi wa Jamii inashiriki na Kunyakua ushindi kwenye tuzo hizi muhimu katika taaluma ya Uhasibu Tanzania.
Akiongea baada ya Kupokea tuzo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amesema ni furaha kubwa kwa Taasisi kutunukiwa tuzo hii ambayo ni kielelezo cha weledi na umahiri wa hali ya juu wa utunzaji wa taarifa za fedha na menejimenti nzuri za fedha za serikali katika Taasisi Yetu.
“Tumekuwa tukitoa huduma ya taaluma ya elimu, na ni manguli wa kutoa na kufundisha katika taaluma ya ustawi wa Jamii lakini sasa tunaonyesha weledi mkubwa katika fani ya uhasibu na utunzaji taarifa za fedha, naipongeza sana timu yangu ya Uhasibu ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiongozwa na CPA Athuman Senzota.” alisema Dkt. Joyce.