Home Biashara Vodacom kuwaunganisha Watanzania wengi zaidi kwenye intaneti katika msimu huu wa Sikukuu

Vodacom kuwaunganisha Watanzania wengi zaidi kwenye intaneti katika msimu huu wa Sikukuu

0

Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Wapili kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Wapili kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali
nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi.

Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Mteja wa Vodacom Elvira Kamuzora (Kushoto) wakati wa uzinduzi wa ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na
kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi.

Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na wapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania
wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi.

***************************************

Desemba 7, 2019 Mwanza. Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inatoa fursa kwa wateja wake kutoa zawadi ya simu ya Smart Kitochi kwa ndugu, jamaa na marafiki wakati wa Msimu huu wa Sikukuu.

 

Hatua hii ya kipekee inalenga kuwawezesha watanzania wengi kujiunga na matumizi ya digitali kama kampuni inayojiendesha kidigitali kwa lengo la kuongeza idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti na kupata habari mtandaoni, kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na inaoaminika zaidi nchini kote.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa hiyo katika Viwanja vya Igoma jijini Mwanza, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom, George Lugata alisema, Wakati wa msimu huu wa Sikukuu Vodacom inatambua kuwa kuna umuhimu wa kutoa zawadi lakini pia kuwaunganisha wapendanao, ndiyo maana ya ofa hii. “Wakati wa msimu huu wa Sikukukuu.

 

Vodacom inatoa fursa ya kipekee kusambaza upendo nchini kote kwa kumiliki au kumpa zawadi ya simu ya Smart Kitochi ndugu, jamaa na rafiki kwa bei nafuu kabisa ya Sh. 45,000 kutoka Vodacom.

 

Katika maono ya kuipeleka Tanzania katika zama za kidigitali, Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kiasi kikubwa imewekeza katika miundombinu ya mawasiliano kupitia mtadao wake wa Supa Network wenye kasi na ambao unawafikia watanzania waliowengi kwa zaidi ya asilimia 92 katika viwango vya 3G, 4G na 4G plus nchi nzima. Hata hivyo jitihada hizi bado zinakwamishwa na uwepo wa matumizi madogo ya simu janja kwa watanzania walio wengi.

 

“Tunataka kila mmoja apate uzoefu wa kutumia mtandao wetu wa Supa Network lakini pia afaidike na huduma ya intaneti. Pata Simu ya Smart Kitochi wewe na umpendaye na Vodacom watahakikisha kuwa unaunganishwa katika kipindi chote hiki cha msimu wa sikukuu kwa kukupa Data yenye GB 24, dakika 500 za muda wa maongezi na SMS 200 bure kwa muda wa miezi sita, vyote kutoka Vodacom. Pia utarejeshewa asilimia 10 kwa kila muamala utakaofanya kupitia MPesa, Naomba Watanzania wengi kujitokeza katika promosheni hii ili
waweze kuunganishwa katika huduma hizo muhimu,” alisema Lugata.

 

Ikiwa na betri yenye nguvu ya 1400mAh ambayo inaiwezesha kukaa kwa muda wa masaa sita ya mazungumzo, Smart Kitochi inatumia laini mbili za simu, lakini pia ni chaguo sahihi kwa watanzania waliowengi katika soko la simu hapa nchini.

 

 

Smart Kitochi ina apps maarufu kama Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram, Google Assistant na nyingine nyingi zitakazomuwezesha mtanzania kuwa katika jamii ya watumiaji wa intaneti.

 

“Wateja wetu wanaweza kupata simu ya Smart Kitochi katika maduka yetu yote ya Vodashop nchi nzima, na kupitia katika magari yetu maalumu wakati wa msimu huu wa sikukuu, matamasha yetu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Arusha, Dodoma,
Mbeya na Dar es Salaam.

 

Msimu huu wa Smart Kitochi unaambatana na matukio kadhaa ya kusisimua kama vile mashindano ya dansi, na burudani mbalimbali za katika mikoa hiyo mitano. Lengo la promosheni ni kuhakikisha kuwa tunawafikia watanzania wengi kwa kuwaunganisha katika maisha ya kidigitali,”

 

Pamoja na ofa hii, Vodacom itakuwa ikifanya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

 

‘Wateja wetu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwa kuzingatia umuhimu wa zoezi hili. alisema Lugata