Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Wananchi wa Kijiji cha Singa, Kata ya Kibosho Mashariki Mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kumuunga mkono Bi. Verdiana Martini Mmasy, mdau wa maendeleo wa kijiji hicho, katika ujenzi wa madaraja ya kudumu.
Wamesema madaraja hayo yatakuwa muhimu katika kuunganisha vijiji mbalimbali katika Kata ya Kibosho Mashariki, Mkoani Kilimanjaro.
Bi. Mmasy, ambaye ni mtaalamu wa maendeleo, ameomba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Miundombinu kushirikiana naye katika ujenzi wa madaraja hayo. Lengo ni kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wakazi wa Kibosho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Singa Kifueni, Ndugu Joseph Ngowi, pia amesisitiza umuhimu wa serikali kuziingatia Kata ya Kibosho, ambayo imezungukwa na Mto Kalanga.
“Sehemu kubwa ya madaraja yaliyojengwa awali yalikuwa ya muda. Mfadhiri Verdiana Martini Mmasy amekuwa mkombozi mkubwa katika kijiji chetu na Kata ya Kibosho kwa kujenga madaraja ya kudumu” amesema Ngowi.