Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizindua Mfumo wa Bodi ya Usajili wa Wathamini wa Kidigitali wakati wa mahafali ya tatu ya bodi hiyo jijini Dodoma tarehe 7 Juni 2024.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza na wajumbe wa Bodi mpya ya Usajili wa Wathamini wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dodoma tarehe 7 Juni 2024. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mhandisi Anthony Sanga na kulia ni Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wathamini Joseph Shewiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Usajili wa Wathamini.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akishuhudia Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Usajili wa Wathamini Zidikheri Mgaya Mudeme (Kushoto) akikabidhiwa taarifa ya bodi hiyo na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake FRV Dkt Cletus Ndjovu wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dodoma tarehe 7 Juni 2024.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya Bodi ya Usajili wa Wathamini wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dodoma tarehe 7 Juni 2024.
…….
Na Eleuteri Mangi, Dodoma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametoa siku 90 kwa Bodi ya Usajili ya Wathamini (VRB) kuzindua mihuri ya Wathamini ya kisasa yenye alama za kidijiti ili wananchi wajiridhishe kazi yao inayofanywa na mtaalam aliyesajiliwa kisheria.
Waziri Silaa amesema hayo Juni 7, 2024 jijini Dodoma wakati wa mahafali ya Wathamini ya tatu ya Bodi ya Usajili wa Wathamini inayosimamiwa na Bodi ya Usajili wa Wathamini.
“Namwelekeza Mwenyekiti wa Bodi ndani ya siku 90 kuanzia leo napenda kuona bodi inazindua mihuri ya wataaalam yenye Barcode kwa maana ya kuwa na alama za ulinzi za kielekroniki ambao utaunganishwa na mfumo wenu wa kutambua Wathamini ili kusimamia misingi ya taaluma na weledi katika kutekeleza majukumu yao.” amesema Waziri Silaa.
Ameongeza kuwa mihuri ya Wathamini itasaidia wananchi wa kawaida kuwatambua wathamini kwa kuwa kila mmoja atakuwa na alama ambazo hazitafanana na mwingine hatua itakayowasaidia kutambua kuwa kazi hiyo imefanywa na mtaalam ambaye anatambulika kisheria na kumchukulia hatua za kinidhamu kama atakiuka taaluma yake na misingi ya kazi yake.
Aidha, Waziri Silaa amewaasa wahitimu wa hao kufanya kazi yao ya Uthamini kwa kumtanguliza na kumheshimu Mungu na kuwatumikia watanzania katika kupata huduma za uthamini kwa haki kwa kufuata misingi ya taaluma na sheria za nchi.
Awali akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. Jerry Silaa wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amewasisitiza wajumbe hao kusimamia taaluma na weledi katika kazi ya uthamini kwa mujibu wa taaluma yao na milango ya wizara ipo wazi wakati wote waendelee kushirikiana ili kuleta maandeleo endelevu kwa taifa na watu wake na kuleta mabadiliko chanya ambayo yataacha alama katika kipindi cha uongozi wao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wathamini Bw. Zidikheri Mgaya Mudeme amemhakikishia Waziri Silaa na Menejimenti ya Wizara ushirikiano wakati wote wa kutekeleza majuku yao hatua itayowasaidia Bodi hiyo kusimamia maadili ya taaluma ya Uthamini.
Mahafali hayo yamehudhuriwa na wahitimu 91 ambao wanatambuliwa na Bodi ya Usajili wa Wathamini ambao wamekula kiapo cha uadilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kwa haki