Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) leo tarehe 07 Juni 2024 amefungua maonesho ya Utalii ya _Karibu Kili Fair 2024_ yanayofanyika katika Viwanja vya Magereza Kisongo Mkoani Arusha.
Takribani makampuni 460 ya utalii, yanayotoa huduma katika tasnia ya utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania zikiwemo taasisi za serikali zinazohusiana na utalii ikiwemo TAWA.
Mhe. Kairuki akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas alitembelea banda la TAWA na kujionea shughuli za utoaji elimu kuhusu Utalii, Uhifadhi na maelezo kuhusu fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA.
Mhe.Kairuki ameipongeza TAWA kwa kutumia vyema maonesho hayo kwa kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji katika sekta ya utalii na pia amehasa hamasa zaidi ifanyike katika kutangaza maeneo yote yanayosimamiwa na TAWA ikiwemo maeneo ya Jumuiya ya hifadhi za jamii.