Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba wakati alipotembelea banda hilo mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANTRADE Dkt Ng’wanza Kamata na katikati ni Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE.
…………………………………………
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema hana wasiwasi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Naibu Waziri Injinia Manyanya amesema hayo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere.
“Sina wasiwasi na ninyi kwa sababu sijawahi kusikia malalamiko yoyote mkilalamikiwa kuhusu utendaji wenu hivyo nina imani na ninyi chapeni kazi” Alisikika akimuambia Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wakati alipokuwa akipata maelezo ya taasisi hiyo.
(TMDA) inashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na taasisi hiyo muhimu nchini katika udhibiti wa ubora wa dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha mlaji anapata huduma ya dawa zenye ubora na viwango viliyowekwa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba huku akisoma kipeperushi wakati alipotembelea banda hilo mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere kushoto ni Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii TMDA.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akisoma kipeperushi huku Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba akifurahia mara baada ya kusikia maneno mazuri kutoka kwa Naibu waziri hukusu TMDA kushoto ni Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii TMDA.
Maofisa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kulia na Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii wakiwa tayari kabisa kwa kupokea Naibu Waziri Injini Stella Manyanya.