Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) , Monica Mutoni (kulia) akizungumza jambo katika warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kuelimisha umma kuhusu kuzuia kuzama maji yaliyotolewa Juni 4, 2024 na Shirika lisilokuea la kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) katika Hotel ya Mbezi Garden jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika lisilokuea la kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) Editruda Lukanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muhimu wa kuandika habari ya kuzuia kuzama maji kwa jamii.
Matukio ya picha mbalimbali.
………………
Shirika lisilokuea la kiserikali la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) limesema kuwa takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 200,000 kwa mwaka wanakufa kutokakana na kuzama maji.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Editruda Lukanga katika warsha ya wanahabari na wadau mbalimbali wa masuala ya Hali ya hewa ikiwemo Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na kusema kuwa kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja ili kutoa elimu ambayo itasaidia kuzuia watu hasa wavuvi kufa maji.
Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanakufa maji kutokana na uzembe, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari ya maji yatokanayo na mvua kubwa, mito, maziwa na bahari kwani kwa kuwa yanaua na kuacha simanzi kwa familia, jamii na Taifa Kwa ujumla.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) , Monica Mutoni amesema wanashirikiana vema na shirika hilo la EMEDO na wadau wengine ili kuzuia watu kupata na changamoto mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.
Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanafanya shughuli zao katika maziwa makuu na ukanda wa bahari ambapo wanakumbana na athari za hali mbaya ya hewa hususani upepo mkali.
Meneja wa maji mradi wa Kuzuia kuzama maji Ziwa Viktoria Arthur Mugema amewashauri watu wanatumia bahari, mito na maziwa wakiwemo wavuvi kuhakikisha wanakuwa na vifaa maalumu vya kuogelea kama vile mambo ya okozi (life Jacket).
Amesema kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwani vinawasaidia wasizame maji wakati vyombo vyao vinapopata hitilafu, huku akiomba Serikali kuona umuhimu wa kupunguza gharama za vifaa ikiwemo life Jacket.
Mugema amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari zilizoko katika Maeneo yaliyoko Kanda ya Ziwa Kwa kuwa walengwa wakubwa ni wavuvi, watoto na akina mama wachakatani wa samaki.