Maelfu ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya zake, wa ngazi za mashina hadi mkoa, na wawakilishi wa makundi katika jamii, kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, wakiwa wamejaa pomoni katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali kuhusu usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025 na uhai wa CCM kuanzia ngazi ya mabalozi, katika mkutano uliofanyika mjini Arusha, Jumatatu, Juni 3, 2024.