*Akagua ujenzi wa maktaba na ukumbi wa mihadhara.
*Aongea na uongozi wa Chuo pamoja na wanafunzi wa chuo hicho
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 03, 2024 amefanya ziara katika chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kivukoni – Kigamboni
Akiwa katika viunga vya chuo hicho amekagua maendeleo ya ujenzi wa Maktaba ambayo kukamilika kwake itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja pamoja na ukumbi wa mihadhara ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu sio chini ya 1000. ujenzi huo unaendelea ijapokuwa Mhe Mkuu wa Mkoa hajaridhishwa na Kasi ya ujenzi huo.
Aidha RC Chalamila alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wa chuo hicho ambapo aliwapatia nasaa za kufikia mafanikio ” Kila aliyoko hapa anaweza kuwa yoyote Kikubwa ni kuto kata tamaa ondoeni dhana ya unamjua nani” Alisema RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila amepokea kero mbalimbali ambazo wanafunzi wa chuo hicho hukabiliana nazo ikiwemo kupokea kiasi cha pesa cha mkopo pungufu na ilivyo katika makubaliano ambapo ameiagiza bodi ya mikopo kufanyia kazi Changamoto hiyo na apatiwa mrejesho.
Sanjari na hilo RC Chalamila ameahidi kufanyia kazi Changamoto zote alizoelezwa ikiwemo kuonana na Waziri mwenye dhamana ya elimu ili kupata Suluhu za Changamoto hizo.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Prof Shadrack Mwakalila amesema chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Pamoja na kutoa fani mbalimbali bado kimeendelea kujikita katika fani za uongozi na maadili na utawala hivyo wanafunzi wanaopita katika chuo hicho wameandaliwa vizuri katika nyanja ya uongozi, maadili na utawala
Mwisho Mhe Albert Chalamila katika ziara hiyo aliambatana na wataalam kutoka Bodi ya Mkopo, Bima ya Afya,na NACTEVET