Na Sophia Kingimali.
Waziri wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Sekta ya Uwekezaji nchini inazidi kuimarika na kufanya uchumi wa nchi kukuwa na kuvutia uwekezaji.
Hata hivyo amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuvutia Uwekezaji na ndio inafanya kampuni za nje kuungana na kampuni zilizopo nchini kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya Uwekezaji na biashara.
Profesa Kitila ameyasema hayo Mei 25,2024 wakati wa hafla ya uzinduzi muunganiko wa kampuni ya Bia ya Heaken na kampuni ya Namibia na kuwa Heinken Beverage itahusishwa vinywaji vya Vileo zaidi ya viwili katika hafla hiyo iliyofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Amesema uwepo wa kampuni hizo nchini unakwenda kuongeza ajira kwa vijana lakini pia mapato ya nchi yataongezeka maradufu.
Hii kampuni ilikuwa inatoa mapato ya kodi ya sh.bilioni 11 sasa wanakwenda kutoa mapato ya kodi ya sh.Bilioni 21 hii ni mara mbili yake ya kodi ya awali lakini pia ajira zinakwenda kuongezeka kwa vijana”,Amesema.
Profesa Kitila amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mikakati ya Uwekezaji ikiwa ni pamoja wadau wote wanaohusika na Uwekezaji kuwa na sauti moja kwenye eneo kuondoa changamoto kwa wanaotaka kuwekeza nchini.
Ameongeza kuwa nchi inakwenda kasi katika Uwekezaji ni pamoja na kuwa na rasilimali watu ya kutosha ambao wanaweza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali.
Aidha Profesa Mkumbo amesema Ofisi mpya ya Heineken nchini tukio hilo linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji
wa Tanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.
” Kujikita kwa
Heineken kwenye soko letu ni dhahiri, na ninatazamia kuona matokeo chanya ya jalada lao jipya iliyopanuliwa kwa uchumi na watu wetu.” amesema
Kwa upande wake Meneja wa Masoko na Biashara Lilian Pascal amesema kuwa wanakwenda kuongeza ajira na ulipaji wa kodi kwani idadi iliyokuwepo ilikuwa ya kinywaji kimoja sasa iko zaidi vinywaji viwili.
Amesema Heineken imepanua wigo zaidi kwa kuzindua bidhaa zake mpya mbalimbali kwenye orodha ya jadala lake nchini Tanzania.
Kampuni inayoongoza duniani ya vinywaji,Heineken imesherehekea upanuzi wake zaidi wa vinywaji na kutangaza bidhaa mpya ikionyesha orodha za aina mbalimbali za chapa zilizoanzishwa nchini Tanzania.
Matokeo ya uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za vinywaji ni baada ya kukamilika kwa ununuzi wa kampuni ya Distell Group Holdings Limited
(Distell’) na Namibia Breweries Limited (NBL).
Nae,Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, amesema kuunganishwa kwa biashara yao hadi kufikia zaidi ya bia ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania na ni kielelezo cha imani yao kama Heineken katika ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini.
Amesema umiliki wa aina mbalimbali za chapa zinazojulikana imewawezesha kutoa jalada kamili la vinywaji ili kukidhi mahitaji yawatumiaji yanayoendeleza kwa upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia na kuongeza ari yao kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji wakidumisha nyakati za umoja wa kweli.
Uzinduzi wa biashara mpya ya Heineken pamoja na bidhaa mpya zinazopatikana
nchini Tanzania ni hatua muhimu kwa Heineken Beverages International na ni sehemu ya mipango yake kupanua biashara na uwekezaji wa kimkakati.