Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watanzania wengi zaidi wamehamia kwenye matumizi ya vifaa vya kisasa vya mawasilianao na kuachana na simu za kianalogia.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa ueneaji wa matumizi ya simu za kisasa miongoni mwa watu uliongezeka kwa asilimia 32.59 mnamo Machi 2024 ukilinganisha na asilimia 32.13 Desemba 2023.
Hii ni ishara nzuri kama taifa kwa upande wa maendeleo ya sekta ya mawasiliano inayochochewa na ukuaji wa uchumi wa kidigitali duniani.
Simu sio tena kifaa cha kifahari ambacho kimekuwa kikitumiwa na watu wenye uwezo pekee bali ni hitaji la muhimu kwa kila mtu ili kufikia usawa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Serikali kwa kushirikiana na makampuni tofauti ya simu na watengeneza vifaa vya mawasiliano zimekuwa zikishirikiana ili kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa bila ya kujali walipo na hali ya vipato vyao.
Katika kuunga mkono jitihada hizi kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwa kushirikiana na wadau tofauti inawawezesha Watanzania kununua simu za kisasa kwa mikopo nafuu.
Akizungumzia kuhusu ushirikiano huo Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania, Manish Jangra amebainisha kuwa siku zote wapo mstari wa mbele kuwarahisishia watu kupata simu za kisasa kwa gharama nafuu ili kusaidia maendeleo ya shughuli za kiuchumi.
“Uhitaji wa simu za kisasa umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwa mujibu wa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi wanafahamu faida zinazopatikana kutokana na kuwa na vifaa hivi vya kisasa. Mawasiliano yameongezeka wigo kutoka kupiga na kupokea simu kwa ndugu jamaa na marafiki mpaka kutumika kwa shughuli za kijamii na kiuchumi za kila siku,” alisema Bw. Jangra.
Tunajivunia ushirikiano wetu na kampuni za simu na mikopo midogo midogo ya fedha, sasa Watanzania wanaweza kutembelea maduka na mawakala wa Samsung na kupata simu za kisasa kwa mikopo nafuu.
“Tunafahamu kuwa watu wengi wanatamani kuwa na simu za kisasa lakini changamoto inayojitokeza mara nyingi ni kuwa na pesa ya pamoja kufanya manunuzi. Hivyo basi kupitia kampeni hii kwa kuanzia na kiasi cha shilingi 70,000/- mteja anaweza kununua simu ya kisasa kwa mkopo nafuu ambao unamruhusu kurejesha kiwango cha chini aidha kwa siku au wiki kwa kipindi cha miezi 12,” alimalizia Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania.
Watanzania wanaweza kunufaika na kampeni hii ambayo inaendesha nchi nzima kwa kutembelea maduka, mawakala, na ofisi za Samsung pamoja na Watu Simu na kujipatia simu za aina ya Samsung Galaxy A05, Galaxy A15, Samsung Galaxy A25 5G, Samsung Galaxy A35 5G, na Samsung Galaxy A55 5G. Kwa kuwa na simu ya kisasa kutakurahisishia shughuli za kila siku kama vile uchumi, fedha, afya, kilimo, elimu, burudani, na kadhalika