Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Waja (MNEC),Eng Chacha Mwita Wambura,amesema ataendelea kuwaunga mkono wazee katika mchezo wa bao ambao umekuwa ukiwakutanisha wazee mbalimbali Mjini Geita.
Mnec Chacha amesema hayo wakati akifunga mashindano ya mchezo huo ambao umefanyika kwenye viwanja vya CCM Wilaya ya Geita,ambayo yameambatana na Zawadi Mbalimbali kama motisha ya kuthamini mchezo huo.
“Wazee wangu wa klabu ya JK Nyerere niwapongeze Sana Mmesema mchezo wa Bao umekuwa ni chanzo pia Cha kumuhenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere,Lakini Mbali na kumuunga umekuwa ni mchezo wa kuwatutanisha na Kujadili masuala Mbalimbali ya maendeleo niwaombe Kupitia mchezo huu tuendelee kusisitiza Maadili mema na kuwafundisha Tabia njema vijana wetu na watoto wetu Tunataka Taifa lenye Watu wenye Maadili na nyie wazee wangu ndio ambao mnaweza kuwasaidia vijana wetu na watoto wetu “Eng Chacha Wambura MNEC.
Aidha, Eng, Chacha Mwita Wambura amewasihi wazee na watanzania wote kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Niwaombe Sana Wazee wa Klabu ya Jk Nyerere, Msemeni na Muungeni Mkono Raisi Samia Kwa kazi kubwa anayoifanya na mwakani panapo majaaliwa kwenye Uchaguzi hakikisheni Geita inaongoza Kwa Kumpa kura Nyingi za kutosha”Eng Chacha Wambura MNEC.
Naye Mzee Julius Mussa amemshukuru Mnec Chacha na kuhaidi kuendelea kushirikiana naye katika Kila hatua kwani jambo ambalo amefanya la kuwakumbuka wazee wacheza Bao ni la kupongezwa na kuingwa na Watu wote ambao wanamapenzi na michezo ya asili.