Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Austria, Mhe. Wolfgang Sokotka, katika Ofisi za Bunge hilo zilizopo Vienna nchini Austria leo tarehe 21 Mei, 2024.
Pamoja na masuala mengine, Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Austria.