Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mhandisi Mohamed Salu akitoa taarifa ya kuanza kwa uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya Mv Clarias kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
…………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeanza kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha kuzama kwa Meli ya Mv Clarias iliyopinduka na kuzama majini katika Ziwa Victoria Mei 19, 2024.
Hayo yamebainishwa leo Mei 20, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mhandisi Mohamed Salu alipokuwa akitoa taarifa ya kuanza uchunguzi wa kuzama kwa Meli hiyo kwa waandishi wa habari.
Amesema taarifa za awali Meli hiyo ilirudi salama ikaenda kirumba Wilaya ya Ilemela ikushusha mizigo na abiria 250 ikarudi kupaki katika bandari ya Mwanza Kusini.
“Wataalamu watafanya uchunguzi wa kuchunguza kitu kimoja baada ya kingine na uchunguzi utakapokamilika tutaijulisha Serikali ili ijue hatua za kuchukua”, amesema Salu
Ameeleza kuwa kwa mashaka ya kufikirika Meli ikiwa imepaki imeweza kunyonya maji na kupelekea kuzama, ndio maana wameita wataalamu ili wachunguze kwanini Meli iliingiza maji.