Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Divid Concar (Kulia) wakishuhudia Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania Innosent Mushi wapili kushoto na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment (BII) Sithembumenzi Vuma (wapili kulia) wakibadilishana hati za mikataba wa kuboresha huduma za mawasiliano nchini kaika hafla ya utiaji saini iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo katika mkataba huo BII imetoa dola za kimarekani milioni 30 kwa ajili ya kujenga minara mipya 200 ambayo italeta tija katika kutatua changamoto ya mawasiliano hasa maeneo ya vijijini.
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiwa na Balozi wa Uingereza nchini Divid Concar (Kulia) wakifurahia baada ya Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania Innosent Mushi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment Sithembumenzi Vuma (wapili kulia) kumaliza kusaini hati za mikataba ya kuboresha huduma za mawasiliano nchini.
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya kusaini ya makubaliano ya kujenga minara kati ya Kampuni ya TOA Tanzania na Taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII).
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa British International Investment Sithembumenzi Vuma akizungumza katika hafla ya kusaini ya makubaliano ya kujenga minara kati ya Kampuni ya TOA Tanzania na Taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII).
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amepongeza jitiada zinazofanya na sekta binfasi ikiwemo Kampuni TowerCo of Africa Tanzania (TOA Tanzania) ambayo imeingia makubaliano na Taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII) kufanya uwekezaji wa dola za kimarekani milioni 30 kwa ajili ya kujenga minara mipya 200 ambayo italeta tija katika kutatua changamoto ya mawasiliano hasa maeneo ya vijijini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kutia saini makubaliano ya kujenga minara kati ya Kampuni ya TOA Tanzania na Taasisi ya Uingereza, British International Investment (BII) ambayo imefanya uwekezaji wa dola za kimarekani milioni 30 kwa ajili ya kupanua miundombinu ya Mawasiliano nchini, Waziri Mhe. Nape Nnauye, amesema kuwa hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa Serikali, huku akieleza kuwa uwekezaji huo unakwenda kuongeza nguvu katika mapinduzi ya nne ya Viwanda.
Mhe. Nnauye amesema kuwa ya uwekezaji utakuwa na tija nchini, huku akieleza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji ili kuongeza chachu katika kukuza maendeleo.
Nae Mtendaji Mkuu wa TOA Tanzania Bw. Innocent Mushi, amesema kuwa makubaliano ya uwekezaji huo yataongeza nguvu ya kufikia malengo ya kupanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuongeza kasi ya kukua kwa huduma za kidijitali nchini Tanzania, huku akiahidi utekelezaji unaozingatia utunzaji wa mazingira pamoja matumizi ya nishati jadifu.
Bw. Mushi amesema kuwa minara hiyo mipya 200 itakayojengwa kutokana na makubaliano waliyosaini itasaidia kuongeza upatikanaji wa mawasiliano Tanzania Bara na Visiwani na kuwaungasnisha watanzania wengi zaidi ambao walikua mbali na huduma ya mawasiliano.
“Makubaliano ya uwekezaji wa fedha na BII yatatuongezea nguvu ya kufikia malengo yetu ya kupanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuongeza kasi ya kukua kwa huduma za kidijitali Tanzania”. amesema Bw. Mushi.
Amesema kuwa kwa hisani ya BII wanakwenda kukuza upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kimtandao kwenye jamii ambazo awali zilizokuwa mbali na huduma, huku akieleza kuwa wamejidhatiti kwenye mazingira endelevu na maendeleo.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, amefurahishwa na makubaliano hayo ambayo yataenda kupanua huduma za mawasilinao nchini Tanzania.
“Tumefurahi kushuhudia utiaji wa saini ya makubaliano haya muhimu kwa BII ambayo yatawezesha upanuzi wa huduma za mawasiliano na kuwafikia watanzania maeneo hadi ya vijijini” amesema Balozi Concar.
TOA Tanzania ni kampuni iliyoanzishwa February 2023 na kujikita kwenye umiliki na kutoa huduma ya kupangisha minara ya simu kwa makampuni ya mitandao ya simu.