Na Fauzia. Mussa. Maelezo.
Afisa mradi wa michezo kwa maenedeleo kutoka TAMWA Zanzibar Khairat Haji amewaomba waandishi wa habari kuibuwa changamoto zinazokwamisha wasichana kushiriki katika michezo ili kuweza kufika sehemu husika na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao, juu usawa wa kijinsia katika micheozo huko Ofisi za Tamwa Tunguu Zanzibar amesema kufanya hivyo kutasaidia kuongeza idadi ya wanawake wanaoshiriki michezo nchini.
Aidha amwaomba kuyatumia vyema mafunzo hayo ili malengo yalivyokusudiwa yaweze kufukiwa.
Amefahamisha kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa waandishi hao kwa lengo la kuhakikisha wa ujumuishi na usawa wa kijinsia katika michezo unapatikana.
Sambamba na hayo amewasisitiza kuitumia vyema mitandao ya kijamii kwani itasaidia kufikisha taarifa hizo kwa watu wengi na kwa muda mfupi.
Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo hayo wameahidi kuandika na kutangaza habari za michezo na jinsia ili kuweza kufikia usawa wa kijinsia katika michezo na kuondokana na mitazamo hasi ya ushiriki wa mwanamke katika michezo.
Aidha wamesema watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili kuongeza idadi ya Waandishi wa habari za michezo na kupata idadi kubwa ya wanawake wanaoshiriki katika michezo mbalimbali.
Mapema waliishukuru Tamwa Zanzibar kwa kuwapatia mafunzo hayo nakuomba kupatiwa mafuzo mengine zaidi ikiwemo ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuzidi kuwajengea uwezo na uelewa wa kutafuta na kusambaza elimu hiyo kwa jamii.
Mafunzo hayo ya siku 5 ni miongoni mwa utekelezaji wa Mradi wa maendeleo ya Michezo Afrika “SPORTS DEVELOPMENT AFRICA, EMPOWERING GIRLS THROUGH SPORTS IN ZANZIBAR” wenye lengo la kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki katika michezo ambaounatekelezwa kwa mashirikiano kati ya TAMWA ZNZ, Chama cha wanasheria wanawake (ZAFELA), CYD chini ya ufadhili wa shirika la michezo la Ujerumani (GIZ).