Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akipanda Miti katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ikiwa ni katika kuadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani ambayo yamefanyika jijini Dar es salaamRais wa Mtandao wa Wanawake Tanzania wanaojihusisha na Mazingira na Uhifadhi (WiNN), Dkt.Anna Mahulu akipanda Miti katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ikiwa ni katika kuadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani ambayo yamefanyika jijini Dar es salaamMkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bi Adelaide Salema (Kushoto)sambamba na Afisa kutoka TFS akiwa ameushika mti kwa ajili ya kuupanda katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ikiwa ni katika kuadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani ambayo yamefanyika jijini Dar es salaamMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizungumza na wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali ambao wameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali akielezea umuhimu wa uwepo wa Makumbusho.Baadhi ya wanafunzi wakishiriki katika zoezi la upandaji wa miti katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ikiwa ni katika kuadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani ambayo yamefanyika jijini Dar es salaam. Picha ya Pamoja ya wadau mbalimbali walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani ambayo yamefanyika jijini Dar es salaam.
…………….,……
NA MUSSA KHALID
Makumbusho ya Taifa la Tanzania imeanzisha mradi wa kituo cha utafiti ili kuhakikisha mikusanyo inayofanyiwa itafiti haipelekwi nje ya nchi bali iwe inafanyikia hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Makumbusho ambayo yaliambatana na upandaji wa miti zaidi ya 100 katika Kijiji cha Makumbusho na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Dkt Lwoga amesema kuwa moja ya lengo la kuwepo kwa Makumbusho nchini ni pamoja na malengo ni kuonyesha na kusimamia mla na desturi ya mtanzania.
Dkt Lwoga amesema kuwa kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “makumbusho kwa elimu na utafiti” ambayo inasaidia kutafakari umuhimu wa Makumbusho katika elimu ya utafiti Kuanzia wanafunzi wanapokuwa shuleni .
‘Mfano leo hii watafiti wanapofanya tafiti kuhusu mambo ya kale ili watoke chapisho bora imezoeleka kupeleka nje ya nchi na kutolewa na tafiti za kimataifa hivyo tumetoa hamasa kwa wataalamu wetu na ndio maana Makumbusho tumeamua kuja mradi wa kituo cha utafiti wa malikale kule Arusha kwa ajili ya ya kufanya utafiti hapa hapa nchini”amesema Dkt Lwoga
Amesema kuwa Makumbusho na Malikale ni eneo muhimu sana katika kuboresha elimu,lakini pia watu wa napaswa kuangalia namna ya kuboresha mitaala ikiwemo tafiti mbalimbali zinazochapishwa ili ziweze kuendana na uhalisia wa historia na Urithi wa Taifa letu.
Kwa upande wake Rais wa Mtandao wa Wanawake Tanzania wanaojihusisha na Mazingira na Uhifadhi (WiNN), Dkt.Anna Mahulu amesema kuwa kutokana na dhima ya Makumbusho mwaka huu imeendana na shughuli wanazozifanya wameamua kushiriki kwa pamoja na wanafunzi kwa kupanda miche 105 ikiwa ni katika kuadhikishwa siku hiyo.
Aidha amesema kuwa ni vyema Elimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi Ili waweze kuwa na uelewa wa kuzifahamu historia ya nchi yao ikiwa ni pamoja na kuyatumza mazingira.
Naye Protas Karia ambaye ni Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Ilala,akimwakilisha Kamanda wa TFS Kanda ya Mashariki amesema siku hii wameitumia kwa kupanda miti wakishirikiana na taasisi ya WINI na Makumbusho Ili kusaidia kuimarisha mazingira kuepukana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioshiriki katika maadhimisho hayo Kelvin Masumbuko na Aida Abdalah kutoka Shule ya Sekondari Temeke na wamesema katika siku hiyo wamejifunza masuala mbalimbali ikiwemo utamaduni na makabila ya watu wa kale pamoja na historia ya watu waliopigani Uhuru wa nchi.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Makumbusho hufanyika kila ifikapo tarehe 18 Mei ya kila mwaka na kwa mwaka 2024 maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu “Makumbusho kwaelimu na utafiti”