Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na (Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania) (TAHLISO) imaandaa Kongamano la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika Mei 20, 2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa JUMIKITA Bw. Shabaan Matwebe amesema JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili undishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo.
Amesema pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani
“Aidha, Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa” Amesema Matwebe
Ametanabaisha kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi na (Information Economics) uchumi wa taarifa .
JUMIKITA inawakaribisha wadau wote kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu litakalofungua fursa mbalimbali kwa wana habari wa mitandao ya kinamii na kukutana na wadau mbalimbali ili kubadilisha na uzoefu na maarifa.