Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw, Benny Mwapaja akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari za wizara ya Fedha mtandaoni leo Mei 13, 2024 mkoani Morogoro.
……………….
Wizara ya Fedha imefanya semina na waandishi wa habari na kueleza kuwa huduma za fedha kwa wastaafu ni bure, Wiara ya Fedha haiombi fedha kwa wastaafu ili wapate huduma ya kulipwa mafao yao huduma hizi zinatolewa bure kabisa kwa mstaafu yoyote yule”
Wizara hiyo imeendelea kueleza kuwa Wastaafu wanatakiwa kuwa makini wakati wanapopigiwa simu na watu wanaojifanya ni watumishi wa wizara ya Fedha na kudai watawasaidia namna ya kulipwa mafao yao wakati wanapoyafuatilia, hao ni Matapeli!.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw, Benny Mwapaja wakati akizungumza na waandishi wa habari za wizara ya Fedha mtandaoni leo Mei 13, 2024 mkoani Morogoro.
Amesema wastaafu wanasumbuliwa na matapeli hivyo tumeona badala ya kushughulika nao kisheria peke yake ni vyema tuendelee kutoa elimu kwa wastaafu kwamba huduma hizo kwa wastaafu zinatolewa bure.
Mstaafu anapokaribia kustaafu mtu sahihi wa kuwasiliana naye kwa ajili ya kushughulikia mambo yake ni Mwajiri wake huyu atawasilisha taarifa zake wizarani na taarifa zake zitapokelewa kwa ajili ya kufanyiwa kazi mafao yake mara anapokuwa amestaafu, Pia wanaweza kuwasiliaa na wizara ili kushughulikia taratibu mbalimbali kwa ajili ya kushughulikia mafao kwa namba 0262-160000 hii ni namba ni bure kabisa.
“Ndiyo maana tumeona kuna umuhimu wa kukutana na ninyi kama waandishi wa habari za wizara ya fedha mitandaoni ili kuwaeleza na kuwapa uelewa namna ambavyo wizara ya fedha inasgughulikia madai ya wastaafu.” Amesema Benny Mwaipaja.
Amesema wizara hiyo inafanya tafiti kutokana na kazi zinazozifanywa na habari za wizara ya fedha zinazoandikwa mitandaoni ndiyo maana utaona kuna wengine walikuwepo katika semina ya mwaka jana lakini mwaka huu hawapo hii ni kutokana na mrejesho wa jinsi wanavyofanya kazi za wizara ya fedha
“Nyinyi wanahabari ni Mhimili wa nne wa nchi kutokana na majukumu yenu kwa taifa kwa sababu wananchi wanawaamini sana na ninyi waandishi wa mitandaoni mko haraka zaidi kwa sababu watu wa magazeti wakati wakichakata habari kwa ajili ya kuchapisha kesho nyie mnakuwa mmeshaposti kazi zenu na habari zimeshaifikia jamii, hivyo tunawapongeza kwa kazi nzuri na tunawasihi muendelee kuelimisha wananchi juu ya kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Fedha