Jamii imetakiwa kubadilika na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake katika malezi ya watoto ili kupunguza wimbi la ongezeko la watoto wa mitaa, wanaoishi katika mazingira magumu na wanaoishi vituoni
Hayo ameyasema wakati wa sherehe za siku yake ya mfanano na tarehe ya kuzaliwa iliyofanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Fonelisco ambapo amesema kuwa kila mzazi anawajibu kwa mtoto wake juu ya malezi, saikolojia, afya, elimu na mahitaji mengine ya msingi na kwamba wazazi na walezi waache kukwepa wajibu huo
“Zamani ilikuwa watoto wote ni wa jamii, Hata unapokosea mkubwa yeyote anaweza kukuonya na isitokee mushkeri wowote, Siku hizi maadili na malezi vimekuwa changamoto ndio maana tuna wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili na ongezeko la watoto wa mitaani. “Alisema
Aidha Dkt Mabula amezitaka familia kuwa na mfumo wa kukaa pamoja na kujadili changamoto zao pamoja na kuzipatia ufumbuzi badala ya kuparanganyika
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa kituo Cha Fonelisco kilichopo kata ya Ilemela Ndugu Edward Barnaba akasema kuwa Mbunge Dkt Angeline Mabula amekuwa mdau mkubwa wa kituo chao na kwamba wakaona ipo haja ya kutambua mchango wake kwa kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa sanjari na kumuombea Mungu na afya njema
Aidha akaongeza kuwa kituo chao kinakabiliwa na changamoto za upungufu wa magodoro, neti na chakula
Katika hatua nyengine watangazaji wa kituo cha Clouds Fm kupitia kipindi cha Leo tena na kampeni ya Malkia wa Nguvu wametoa fursa kwa kituo hicho cha kulelea watoto kufika redioni na kuelezea changamoto zao ili wa Tanzania waweze kuwasaidia
Mbunge Dkt Angeline Mabula ameahidi kuwapatia magodoro yote yanayohitajika katika kituo hicho pamoja na kuongoza changizo ambapo fedha taslimu, ahadi ya vitu mbalimbali ikiwemo neti, mafuta ya kupikia vilipatikana