Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela amewataka Vijana kuwa waadirifu pindi wanapoomba na kupewa mikopo inayotokana na asilimia kumi za mapato ya ndani ya halmashauri inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, Vijana na wenye ulemavu kwa kufanyia shughuli za maendeleo uzalishaji mali na kurejesha kwa wakati
Rai hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa shina la Vijana wa UVCCM Sabasaba kata ya Ilemela ambapo amesema kuwa Serikali imekuwa ikitoa fursa mbalimbali Kwa Vijana katika kuwawezesha kujikwamua kiuchumi lakini changamoto kubwa ni uadirifu na uaminifu pindi Vijana hao wanapoaminiwa ikiwa ni pamoja na kutorejesha mikopo wanayoikopa halmashauri
‘.. Serikali inatoa mikopo kupitia halmashauri yetu lakini sasa baada ya mikopo ile haya makundi mengine yanarejesha Ila sisi Vijana tukipewa tunaanza kugombana, vikundi vinakufa na wengine hawarejeshi, nadhani tuwe waadirifu na waaminifu ili kesho tuweze kukopesheka tena..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula amepokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani walioamua kujiunga na chama cha mapinduzi kupitia mkutano huo pamoja na kuwaunga mkono wafanya biashara wa kahawa walio jirani na eneo hilo kwa kuwawekea mabenchi ya kukalia na ununuzi wa vifaa vya kuandalia biashara yao, kuwakabidhi jezi vijana wa kijiwe hicho cha bajaji
Nae diwani wa kata ya Ilemela Wakili Wilbard Kilenzi mbali na kumpongeza Mbunge huyo kwa kazi nzuri anayoifanya akawahakikishia Vijana wa kijiwe hicho kuungana na Mbunge katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili
Zakaria Charles ni mwenyekiti wa shina la Vijana hao waendesha bajaji Sabasaba ambapo amemshukuru Mbunge huyo kwa namna anavyowasaidia Vijana ktk Jimbo lake na kwamba wataendelea kumuunga mkono kuhakikisha changamoto za Vijana zinatatuliwa huku Geoffrey Laurent Kimune
aliyekuwa KADA wa chama cha CHADEMA kata ya Buzuruga na mratibu wa maandamano ktk eneo hilo akifafanua kuwa ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali na kwamba kero na changamoto zote walizokuwa wanapigia kilele zimeweza kutatuliwa hivyo kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hasan na kwamba watamuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao