Wananchi wakipata huduma ya usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
Mwananchi akisajili laini ya simu kwa alama za vidole moja ya Kampuni ya huduma za Simu za Mkononi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi wa Babati.
Wananchi wakihudumiwa usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa TCRA uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Emelda Salum akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wa Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi ya Magugu ya usajili wa Laini za Simu kwa Alama za vidole.
*************************************
Wakazi wa wilayani Bahati mkoani Manyara na viunga vyake wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na kuongeza kuwa ambaye hatatimiza matakwa ya kisheria ya kusajili laini ya simu kwa alama za vidole laini hiyo itafungw
Kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati katika Stendi ya mabasi ya Zamani ya Magugu Mkuu wa Kanda ya Kasikazini wa TCRA Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa Babati na maeneo Mbalimbali wamefika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Magugu kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA na kuweza kusajili laini ya simu kwa alama za vidole.
Mhandisi Salum Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ikiwa kila mwananchi aweze kuwa na namba ya Kitambulisho au Kitambulisho cha Taifa kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.
Amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja kwa huduma za mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni 27 mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.
Hata hivyo amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.
Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.
Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia wananchi kuhakikisha kila mwananchi anasajili laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho.
Salum amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa kupitia Kampeni ya Mnada kwa mnada.
Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 kwa kufika katika maduka ya watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.
“TCRA tutahakikisha tunawafikia wananchi wote kupata elimu ya utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema Mhandisi Salum.
Ameongeza kuwa Kampeni iko katika mikoa yote iliopo katika kanda ya Kaskazini.
Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi kuangalia namba vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na wengi wamepata namba hizo na kufanya usajili kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata utaratibu wa vitambulisho vya Taifa.