Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Alfred Mimata akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho wakati akitoa mafunzo ya usalama wa kimtandao (Cyber Security) yaliofanyika leo Mei 10, 2024 katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam – Tegeta.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam – Tegeta Stella Sarakikya akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho leo Mei 10, 2024 wakati akifungua mafunzo ya usalama wa kimtandao (Cyber Security) kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakichangia mada wakiwa katika mafunzo ya usalama wa kimtandao (Cyber Security) yaliofanyika leo Mei 10, 2024 katika Chuo hicho Ndaki ya Dar es Salaam – Tegeta.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam – Tegeta wakiwa katika mafunzo ya Usalama wa kimtandao (Cyber Security)
…….
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wamepewa mafunzo ya usalama wa kimtandao (Cyber Security) kwa ajili ya kuwasaidia kujilinda na uhalifu wa kimtandano pamoja na kuhakikisha wanakuwa na uwelewa mkubwa jambo ambalo litasaidia kufanya vizuri katika masomo yao pamoja na kuwa watendaji wazuri baada ya kumaliza masomo yao.
Akizungumza leo Mei 10, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mafunzo ya Usalama wa kimtandao (Cyber Security) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Chuo Kikuu Mzumbe wa Ndaki hiyo Bw. Alfred Mimata, amesema kuwa ni muhimu wanafunzi wakawa na elimu ya kijikinga na Uhalifu wa kimtandao ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao pamoja na kujilinda.
Bw. Mimata amesema kuwa lengo la mafunzo hayo wanafunzi wajue maana ya usalama wa kimtandao na namna ya kujikinga ili wasiweze kupata madhara katika masomo.
“Teknolojia inabadilika kila siku, leo tumewafundisha namna ya kujikinga na madhara ya uhalifu wa kimtandao, jinsi wanavyoweza kupata matatizo ya kimtandao kama hawajawa makini pamoja kuepuka miteko ya kimtandao” amesema Bw. Mimata.
Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Stella Sarakikya, ameishukuru Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na uongozi wa Chuo kwa kuwapatia elimu ya Usalama wa kimtandao ambayo inakwenda kuwa msaada katika masomo.
“Tunashukuru kwa kupata mafunzo ya kujilinda na link ambazo zipo kwa ajili ya kuiba nyaraka mbalimbali, elimu hii inakwenda kutusaidia kulinda taarifa zetu muhimu katika simu pamoja na kompyuta” amesema Sarakikya.