NJOMBE, Madaktari bingwa 30 waliowasili mkoani Njombe tayari wameanza kutoa huduma katika Hospitali za wilaya zote mkoani Hapa huku wito ukitolewa kwa wananchi kujitokeza kupata matibabu.
Madaktari Hawa ambao wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwemo Hospitali ya mji wa Njombe Kibena wamefanya upasuaji na huduma nyingine za matibabu bingwa na Kisha kudai kwamba kundi kubwa la Wagonjwa waliofika kufata matibabu ni wanawake ,watoto na uzazi
Erenestina Mwipopo Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Watoto anasema tayari ameanza kuwahudumia watoto na baadhi ya aliowahudumia ni wenye magonjwa ya Moyo,Kuzaliwa kabla ya wakati pamoja na Changamoto nyingine.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wamefika kupatiwa huduma ni pamoja na Grace Mlowe ambae anasema yeye amemleta Mwanae mwenye tatizo la moyo na kwamba alitakiwa kumpeleka Muhimbili lakini ameshinwa hivyo ujio wa Madaktari hao umekuwa msada kwao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena Dokta Ayub Mtulo anasema ni fursa kwa wananchi wa Njombe kujitokeza katika Hospitali za Wilaya zinakopatikana huduma hizo kwani wataalamu hao wapo mkoani hapa kwa muda wa Siku tano pekee.
Magonjwa yanayohitaji huduma za Kibingwa yamekuwa na gharama kubwa jambo ambalo wananchi wa hali ya kawaida wamekuwa wakishindwa.