Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Dkt. Ibrahim Mwangalaba (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Namoto Yusufu Namoto wakisaini Mkataba wa makubaliano wa mradi wa kwanza wa Ununua Viwanja vya Wamachinga wa Soko wa Kariakoo vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani pwani (Machinga Plot Finance) katika hafla fupi iliyofanyika leo Mei 7, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Dkt. Ibrahim Mwangalaba akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 7, 2024 jijini Dar es Salaam kuhusu mradi wa kwanza wa Ununua Viwanja vya Wamachinga wa Soko wa Kariakoo vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani pwani (Machinga Plot Finance).
Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Namoto Yusuf Namoto akizungumza na waandishi wa habari wakatiwa kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa kwanza wa Ununuzi wa Viwanjaa vya Wamachinga wa Kariakoo jinini Dar es Salaam leo Mei 7, 2024 kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba.
Mmiliki wa Ardhi iliyopo kijiji cha Magoza Mkuranga Mkoani Pwani, Bw. Kondo Maulid Mkangala (kushoto) akitia saini ya makubaliano ya kuuza eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za Wamachika Soko la Kariakoo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Urasimishaji wa ardhi inayojulikana kwa jina la Semsic Land Consultant Limited Bw. Seme Nino akitia saini ya makubaliano kwa ajili ya kupima viwanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dkt. Ibrahim Mwangalaba Kushoto na Mwenyekiti wa Machinga Dar es Salaam, Namoto Yusuf Namoto wakionesha mikataba mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa kwanza wa Ununuzi wa Viwanjaa vya Wamachinga wa Kariakoo
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Maendeleo Benki imesaini Mkataba na viongozi wa Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) na Mmiliki wa eneo katika kijiji Magoza Mkoani Pwani kwa ajili ya kuwawezesha wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam kupata viwanja vya bei nafuu isiyozidi milioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 7, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba wa mara ya kwanza kwa ajili ya kununua Viwanja katika eneo lililopo Mkuranga Mkoani pwani (Machinga Plot Finance), Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Dkt. Ibrahim Mwangalaba, amesema kuwa lengo la benki kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kumiliki viwanja pamoja na nyumba.
Dkt. Mwangalaba amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya benki kupokea maombi kutoka kwa KAWASSO kuhusu kuwakopesha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo wamekubaliana kuanza kununua viwanja vya Wamachinga 500 wa Dar es Salaam ili waweze kumiliki ardhi na hatimaye kupata makazi ya kuishi.
“Wamachinga watapa viwanja vya bei nafuu isiyozidi shilingi milioni moja kwa kila kiwanja, huku wakirejesha kidogo kidogo kwa muda wa miezi miwili, awamu ya pili tutaaza kutoa mikopo ya ujenzi wa makazi bora kwa hawa wanufaika kupitia mkopo wa nyumba (Housing Microfinance Loans)” amesema Dkt. Mwangalaba.
Dkt. Mwangalaba amefafanua kuwa umoja huo tayari wameshapa umeshapata hekari 89 katika kijiji cha Magonza Kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, hivyo kutokana na Changamoto inayowakabiri Wamachinga kutokuwa na dhamana zinazowawezesha kupata mikopo kupitia taasisi za fedha Maendeleo Bank imeona na kuitatua changamoto hiyo.
“Kupitia Mpango huu benki itatoa mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa Wamachinga wa Kariakoo kwa awamu ya kwanza ya Mradi ili kuwezeaha kumiliki Viwanja, hivyo pesa hizo ni kwaajili ya ununuzi wa Ardhi, Usafishaji wa eneo husika, Upimaji wa Viwanja pamoja na urasimishaji ili kuwezesha mgawanyo wa viwanja kwa wanachama binafsi ili kila mnufaika aweze kuwa na hati miliki ya kiwanja Chake.” amesema Dkt. Mwangalaba.
Dkt. Mwangalaba amesema kuwa kwa awamu ya pili kwa kushirikiana na KAWASSO na umoja wa Machinga Dar es Salaam, Maendeleo Bank itatoa mkopo wa Nyumba wenye masharti nafuu na gharama ndogo ili kuwezesha Wamachinga kumiliki nyumba ya ndogo yake.
Ameeleza kuwa mpango huo utakapokamilika utawawezesha Wamachinga kumiliki ardhi na Makazi bora pia kutawaongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji ya biashara zao na kuondoa kikwazo cha cha kutokukopesheka kwenye taasisi za fedha.
Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Namoto Yusufu Namoto ameishukuru Maendeleo Benki kwa kuwashika mkono na kuwasaidia kwa kuwapa mikopo ambao utawasaidia kumiliki viwanja pamoja na makazi bora.