Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge akizungumza na wageni kutoka nchini Sierra Leonne ambao
walitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo
zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa
katika matibabu ya moyo barani Afrika. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali ya
Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed Kenneth.
Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed
Kenneth akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya wajumbe kutoka
nchini humo ambao walitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo
kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na
kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo
barani Afrika.
Msimamizi wa wodi ya watoto ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Afisa Uuguzi Theresia Tarimo akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra
Leonne huduma wanazozipata watoto waliolazwa katika wodi hiyo wakati wageni
hao walitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua
kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar
Group Dkt. Tulizo Shemu akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka nchini
Sierra Leonne na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) mara baada ya kumaliza
ziara yao ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo
pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu
ya moyo barani Afrika.
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne
huduma zinazotolewa katika kliniki na wodi za watu maalumu na wagonjwa
kutoka nje ya nchi wakati walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona
huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza
namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani
Afrika.