Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini, Mhandisi Florence Mwakasege (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi zawadi ya Luninga pamoja na Friji kwa wafanyakazi bora wenye Mikataba ya kudumu pamoja na wale wa muda maalum katika hafla katika hafla fupi ya kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika leo Mei 1, 2024 katika Hotel ya Lion Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini, Mhandisi Florence Mwakasege akizungumza jambo na wafanyakazi wa TANESCO wa mkoa huo katika hafla fupi ya kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika leo Mei 1, 2024 katika Hotel ya Lion Jijini Dar es Salaam.
Zawadi ya Luninga pamoja na Friji ambazo wapewa wafanyakazi bora wenye Mikataba ya kudumu pamoja na wale wa muda maalum wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini.
Picha za matukio mbalimbali katika hafla fupi ya kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyokwenda pamoja na utoaji wa Tuzo kwa wafanyakazi bora iliyofanyika katika Hotel ya Lion Jijini Dar es Salaam,
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini imetoa Tuzo kwa watumishi wake waliofanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wafanyakazi wote katika shirika wenye mikataba ya kudumu pamoja na wale wa muda maalum.
Akizungumza leo Mei 1, 2024 katika hafla fupi ya kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyokwenda pamoja na Utoaji wa Tuzo kwa Watumishi Bora, yaliofanyika katika Hotel ya Lion Jijini Dar es Salaam, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini, Mhandisi Florence Mwakasege, amesema kuwa Mkoa unatambua mchango wa wafanyakazi wote katika shirika.
Katika sherehe hizo Mhandisi Mwakasege ametoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi tisa ya Luninga na Friji kwa wafanyakazi sita wenye Mikataba ya kudumu kutoka Ofisi ya Mkoa Kinondoni pamoja na Wilaya zake za Kimara na Kibamba.
“Mkoa umeweka utaratibu mzuri wa kumpata mtumishi bora ambapo wafanyakazi wa TANESCO wa Mkoa huu wanapata fursa ya kupendekeza jina la mfanyakazi mwezake ambaye anaona anastahili kupata tuzo, utaratibu ambao ni rafiki kwa kila mtumishi” amesema Mhandisi Mwakasege.
Mhandisi Mwakasege amewakumbusha watumishi kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku jambo ambalo litasaidia kufikia malengo ya Shirika ya kuendelea kutoa huduma bora ya umeme kwa wateja.
Amewataka watumishi wote kutumia siku hiyo kama chachu ya kuhakisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia wateja kwa wakati.
Nao Wafanyakazi TANESCO Mkoa Kinondoni Kusini wameupongeza uongozi Mkoa pamoja na Tawi la Tuico Mkoa wa Kinondoni kusini kufanikisha sherehe hiyo na kuhakisha wafanyakazi wote wanatambuliwa kwa mchango wao katika mkoa, kwa inatoa faraja kujisikia kudhaminiwa.
Wamempongeza Meneja wa Mkoa huo Mhandisi Mwakasege kwa ubunifu anaofanya katika usimamizi na utekelezaji wa majukumu yake kwa uweledi na kuleta tija kwa Shirika.
Wafanyakazi wameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi ili kuhakisha wateja wanapata huduma bora wakati wowote ili kuleta matokeo chanya kwa Shirika.