Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Makamu wa Rais Philip Mpango amepongeza TUCTA kwa maandalizi mazuri ya meimosi huku akiwataka wafanyakazi hao kusaidiana katika maboresho mbalimbali ya maslahi ya wafanyakazi kwani hatua hiyo utasaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
“Timu ya serikali iliyopo mkoani Arusha imesikiliza kwa makini risala ya wafanyakazi na tunaahidi kulifanyia kazi “amesema Mpango.
Amefafanua kuwa ,kodi ya kima cha chini cha mshahara katika utumishi wa umma tayari serikali imeunda bodi mpya kwa ajili ya kushughulikia hizo changamoto.
Amesema kuwa ,tayari serikali wameanza kufanya utafiti wa kima cha chini cha mshahara katika.sekta binafsi na kuomba TUCTA kutoa ushirikiano na kushirikiana katika mchakato huo.
Wafanyakazi wanaoajiriwa kupitia njia zote wanahitaji kupatiwa haki zote za msingi kama ilivyo kwenye ajira.