Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi, Florence Mwakasege (wa pili kutoka kulia) akiwa katika matembezi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Saaam.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakishiriki maandano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani.
Gari la TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini likiwa limebeba mitambo ya umeme likipita katika Uwanja wa Uhuru katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Picha za matukio mbalimbali
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini limeungana na watumishi wote Duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo : Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga ya Hali Ngumu ya Maisha.
Akizungumza na Mwandishi wetu akiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru uliopo Jijini Dar es Salaam, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi, Florence Mwakasege amesema kuwa maadhimisho hayo ni chachu kwa watumishi wa TANESCO katika kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa huduma bora.
Mhandisi, Mwakasege amesema kuwa lengo ni kutoa huduma ya umeme ya uhakika kwa kuhakikisha inapatikana muda wote ili kuleta maendeleo kwa Taifa.
Amesema kuwa Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini wapaswa kuendelea kuwahudumia wataje kwa kufata uadilifu na maadili ya kazi ili kufikia malengo tarajiwa ya Shirika.
“Tunaendelea kudumia wateja kwa moyo kwa kufata uadilifu wa kazi, naomba kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ya utendaji” amesema Mwakasege.
Amesema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa tanesco katika mkoa huo kuacha tabia ya kufanya kazi mazoea na badala yake wahakikishe wanachapa kazi kwa bidii bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Mhandisi, Mwakasege amesema katika kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa bidii wamekuwa na utamaduni wa kutoa zawadi kila mwaka kwa watumishi bora pamoja na kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa kuwapa moyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Katika maadhimisho hayo Taasisi mbalimbali zimeshiriki pamoja na viongozi ngazi ya Mkoa, huku Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salamm Mhe. Albert Chalamila.