Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman Akipokea sadaka ya tende kutoka kwa Balozi wa Saudia Nchini Tanzania iliyotolewa na taasisi ya misada ya kibinaadamu ya mfalme Salman wa Saudia Arabia,huko Sheria house Mazizini Mjini Zanzibar.
Balozi wa Saudia Nchini Tanzania Yahya Ahmad Okeish Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya sadaka ya tende kutoka taasisi ya misada ya kibinaadamu ya mfalme Salman wa Saudia Arabia huko Sheria house Mazizini Mjini Unguja.
Katibu Mtendaji kamisehni ya Wakfu na mali ya Amana sheikh Abdalla Talib Abdalla akitoa neno la shukrani Kwa Balozi wa Saudia Nchini Tanzania na ujumbe wake mara baada ya kupokea sadaka ya tende kutoka kwa taasisi ya misada ya kibinaadamu ya mfalme Salman wa Saudia Arabia huko Sheria house Mazizini Mjini Unguja.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman akibadilishana mawazo na Balozi wa Saudia Nchini Tanzania Yahya Ahmad Okeish wakati wa makabidhiano ya sadaka ya tende iliyotolewa na taasisi ya misada ya kibinaadamu ya mfalme Salman wa Saudia Arabia,huko Sheria house Mazizini Mjini Zanzibar.
…………………….
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman amepokea tani 25 za tende kutoka taasisi ya misada ya kibinaadamu ya mfalme Salman wa Saudia Arabia .
Akizungumza mara baada ya kupokea sadaka hiyo huko Sheria house Mazizini Mjini Unguja Waziri Haroun amesema Serikali imekua ikipokea misaada mbalimbali kutoka Nchi hiyo ikiwemo nyama na tende kutokana na mapenzi, umoja na mashirikiano yaliopo baina ya Tanzania na Saudia arabia.
Hivyo Waziri Haroun ameahidi kuendeleza kudumisha umoja na masharikiano yaliopo baina ya Nchi mbili hizo kwa maslahi ya wazanzibari na Taifa kwa ujumla.
“Mapenzi baina ya nchi mbili hizi yanazidi kuiimarika siku hadi siku hasa upande wa Zanzibar, kupewa tani 25 kati ya 75 zilizotolewa kwa Tanzania yote ni jambo linalodhirisha upendo, kwaniaba ya Serikali tunamshukuru Mfalme wa Saudia kwa sadaka hii na tunaahidi kuyadumisha mapenzi haya” alieleza mwalim Haruna.
Kwa upande wake Balozi wa Saudia Nchini Tanzania Yahya Ahmad Okeish amesema jumla ya tani 75 za tende zimetolewa na Mfalme wa Saudia kama sadaka kwa Nchi ya Tanzania ambapo tani 25 ni kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar, 25 Tanzania bara na 25 kwaajili ya watu maalum ikiwemo wakimbizi.
Alieleza kuwa mapenzi yaliopo kati ya Nchi mbili hizo yamesababishwa na undugu wa dhati uliopo kati ya Tanzania na Saudia unaolinganishwa katika mambo mbalimbali ikiwemo tabia ,silka, tamaduni na hata desturi za Nchi hizo.
Mapema Balozi Okeish amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na sheria Mwalimu Harun Ali Suleiman kwa hatua walizochukua hadi kuhakikisha sadaka hiyo inaingia Zanzibar pamoja na Taasisi zote zilizosaidia kufanikiwa kwa kufika sadaka hiyo Nchini.
Nae Katibu Mtendaji Kamisehni ya Wakfu na mali ya Amana Sheikh Abdalla Talib Abdalla ameishukuru Serikali ya Oman kwa sadaka hiyo na kuahidi kuwa itawafikia walengwa.
Amefahamisha kuwa miongoni mwa majukumu ya kamisehni hiyo ni kupokea na kugawa sadaka kwa wenye uhitaji hivyo amesema kwa kushirikiana na taasisi za kidini sadaka hiyo itagaiwa kwa kila anaestahiki.
“Sadaka hii tutaipeleka katika familia mbalimbali zenye uhitaji,mahospitalini ambako kuna wagonjwa wetu, vituo vya kulelea watoto yatima na vituo vya kutunzia wazee katika Shehia zote za Unguja na Pemba” alieleza sheikh Abdalla.