Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, Nikolai Patrushev (wa kumi na tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani ya nchi 20 Duniani waliokutana nchini Urusi katika Jiji la St.Petersburg kujadili changamoto ya uhalifu wa kimtandao na jinsi ya kupambana nao.Tanzania pia inashiriki mkutano huo ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akionyeshwa jinsi ndege isiyo na rubani inavyoweza kupambana na uhalifu na Afisa kutoka Kampuni ya DOMINA,Alexeen Alexander wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini UrusiPicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(wapili kushoto) wakisikiliza ufafanuzi wa programu maalumu ya kudhibiti uhalifu wa Kimtandao kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya SOLAR,Timul Solovev wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyio, Miriam Mmbaga(katikati) wakisikiliza maelezo ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Kupambana na Uhalifu wa Kimtandao(CyberED),Gadzhi Akhmedov wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(kulia) wakionyeshwa jinsi Mfumo wa Kudhibiti Uhalifu wa Kimtandao unavyofanya kazi na Mtaalumu wa Teknolojia ya Habari kutoka Kampuni ya KOMIB,Egor Bogomolov wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………
Na Mwandishi Wetu,URUSI
Serikali imedhamiria kushirikiana na nchi ya Urusi katika kudhibiti uhalifu nchini ikiwemo uhalifu wa mtandao ambao umeanza kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiweka wazi dhamira ya kujengewa uwezo kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na nchi zilizoendelea kiteknolojia katika kudhibiti uhalifu huo unaotajwa kuvuka mipaka.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama unaoendelea nchini Urusi ambao ulifunguliwa na Rais wa Shirikisho la Urusi na kuongozwa na Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, Nikolai Patrushev.
‘Katika kudhibiti masuala ya uhalifu wa kimtandao matumizi ya teknolojia hayaepukiki ndio maana serikali imeona kuna haja ya kuimarisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ujuzi kwa askari wetu sasa kupitia mkutano huu tunaenda kujenga mahusiano kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Jeshi la Polisi la Urusi ili tuweze kudhibiti uhalifu wa kimtandao ambao umekua ukisababisha madhara mbalimbali katika jamii ikiwemo ya kiusalama,kiuchumi na hata maadili’. Alisema Waziri Masauni
Akizungumza wakati wa Mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Miriam Mmbaga alisema muelekeo wa wizara katika kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ina mkakati maalumu wa kuwajengea uwezo askari waliopo katika Vyombo vya Ulinzi hasa katika masuala ya teknolojia huku akiweka wazi juu ya suala la ajira pia kuweka kipaumbele kwa watu waliosomea masuala ya teknolojia ya Habari.
Mkutano huo wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama umehudhuriwa na nchi takribani 20 huku msisitizo zaidi ukiwekwa katika kupambana na uhalifu wa kutumia teknolojia ambao umekua ni tishio katika mataifa mbalimbali