Na Lucas Raphael,Tabora
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anatarajia kuwa Mgeni Rasmi Siku ya Malaria Dunia itafanyika mkoani Tabora Aprili, 25 mwaka huu katika uwanjwa wa shle ya sekondari Uyui mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa Semina ya waandishi wa habari mkoa wa Tabora iliyofanyika jana mkoani hapa na kufanyika katika ukumbi wa ofisini wa mkoa wa Tabora, Mratibu wa Malaria na mkoani hapo Dkt. Nassoro Kaponta, alisema Mkoa wa huo umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Siku ya Malaria lakini kitakwimu mkoa huo hauna hali nzuri ya Ugonjwa wa Malaria.
Alisema kwamba waziri huyo hatakuwasili katika viwanja hivyo na kukangua mabanda kasha kuzungumza na wanaanchi mbalimbali watakaofika hapo.
Dkt Kaponta alisema kwamba mkoa wa tabora umepewa nafasi hiyo kwa ;enngo la kuhamasisha wananchi na jamii kuweza kupambana vita dhidi ya Malaria katika mkoa huo unao ongoza kwa asilimia 23.4.
Hata hivyo waandishi wa habari mkoani Tabora walipatiwa Semina juu ugonjwa huo hivyo ni muhimu kwa waandishi hao kuweza kuuseme umma juu ya maradhi hayo hata nchini
“Tutumie fursa hii kama vyombo vya Habari, kwani asilimia hizi 23 tunazo husishwa nazo hazina afya kwa mustakabali wa mkoa wetu” alisema Dkt Kaponta.
Aidha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tabora wadhamiria kufanya kampeni kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria na kushusha kiwango cha maambukizi hadi asilimia 8 kutoka Asilimia 23.4 ya sasa.
Mwandishi Dotto Elias ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Habari la Taifa (TBC) alisema nilazima kila mwanahabari wa mkoa huo awiwe kuona ukumbwa wa tatizo na kuiunga mkono Serikali kuhakikisha kiwango hicho kinashuka.
“Mmesikia hapa wenzetu wa Manyara wapo asilimia 0% kwa nn sisi Tabora tushindwe,? Alihoji Dotto
“Ifahamike kuwa Malaria inaongoza kwakukwamisha shughuli nyingi za maendeleo hata kusababisha hasara ya asilimia 1% katika pato la Taifa, hii haina taswira nzuri ni vema tuuunganishe nguvu kwakuwa na vipindi vya elimu kwa umma maslahi mapana ya nchi yetu.