Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jioni ya leo Jumatatu Aprili 22, 2024, ameshiriki akiwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Siku Moja wa Ramani ya Uwekezaji wa Malengo ya Sheria ya Umoja wa Mataifa, hapa Zanzibar.
Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, hapo Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja, ambapo Mheshimiwa Othman amemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Viongozi wa Serikali, Dini, Vyama vya Siasa, Wasomi na Wanataaluma, Wanadiplomasi, Asasi za Kiraia na Wawakilishi kutoka Mashirika mbali mbali, Wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchi, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamehudhuria hapo, wakiwemo Waziri wa Wizara ya Nchi ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Sharif Ali Sharif; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma; Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Soraga na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Shigeki Komatsubara.
Hafla hiyo pia, imeshuhudia Utoaji wa Zawadi kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchi, kutokana juhudi zao za Kuimarisha Sekta hiyo muhimu ya Uchumi hapa Nchini, hatua ambayo imeambatana na burudani kutoka kwa Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Polisi.