Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dkt. David Mathayo David, Ambaye pi Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madin Amesema kwa niaba ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, amempongeza Mheshimiwa Rais kwa jitihada zake za kuendeleza miradi ya nishati.
Katika kipindi cha miaka mitatu, zaidi ya shilingi trilioni 8.18 zimetolewa kwa ajili ya miradi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Dkt. David ameeleza kuwa juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho ya nishati yaliyofanyika Dodoma. Maonesho hayo yalilenga kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.
Tayari Tanzania imeanza kutumia umeme kutoka kwenye Bwawa la Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP), jambo ambalo Dkt. David anataja kama ushindi mkubwa na kielelezo cha kazi nzuri inayofanywa na serikali.
Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt. David anapongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayofanyika kukamilisha miradi mbalimbali ya nishati ya umeme nchini.
Anasisitiza umuhimu wa kumpongeza Rais, hasa katika sekta ya nishati ya umeme. Anafafanua kuwa Leo , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshuhudia majaribio ya treni ya umeme kwa mara ya kwanza, ambayo imeanzia Dar es Salaam hadi Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Hii ni hatua muhimu katika kutumia nishati ya umeme, na ni ishara ya maendeleo katika sekta hiyo, kama alivyobainisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi.