Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambapo imekwenda na Kauli Mbiu isemayo wahudumu wa Afya ngazi ya jamii Nyumba kwa Nyumba hatuachi Mtu Mpaka kieleweke’ambago imefanyika katika ubumbi wa Anartoglo katika Jiji Hilo.
Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto akikabidhi vitendea kazi kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jami.
Picha ya Pamoja,Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto, na wahudumu wa Afya katika Jiji Hilo wakati wa hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambapo imekwenda na Kauli Mbiu isemayo wahudumu wa Afya ngazi ya jamii Nyumba kwa Nyumba hatuachi Mtu Mpaka kieleweke.
………………….
NA MUSSA KHALID
Takriban wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii 200 katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wametakiwa kuendelea kuonyesha juhudi katika kuwahudumia wananchi katika Maeneo yao Ili kuweza kuwaondolea changamoto mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambapo imekwenda na Kauli Mbiu isemayo wahudumu wa Afya ngazi ya jamii Nyumba kwa Nyumba hatuachi Mtu Mpaka kieleweke.
Kumbilamoto licha ya kuwapongeza wahudumu hao wa Afya kutokana na kuanza kazi kwa kujitolea amesema kuwa ni vyema wakaendelea kuwasaidia wananchi wa ngazi ya Chini.
“Hawa wahudumu wetu wanavifua kwa sababu hawatoi siri za wagonjwa wanaowasaidia jambo ambalo linaendelea kuongeza uaminifu naona yao”amesema Kumbilamoto
Awali Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Zaitun Hamza amesema kuwa wahudumu wa Afya wanatembea kifua mbele kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele sekta ya Afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu uchumi na Huduma za Kijamii katika Jiji la Dar es salaam Saad Khimji amesema wataendelea kujadili namna ya wahudumu hao kunufaika na shughuli zao kwani wanajitoa na kunusuru mambo mengi kwenye jamii.
Nao baadhi ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii akiwemo Abdallah Ngobedi pamoja na Masha Abdallah Jumbe wameipongeza serikali kwa kuonyesha umuhimu kwenye sekta hiyo kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitakwenda kuwasaidia katika shughuli zao.